Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wamepanga kufanya ziara ya kihistoria mkoani Morogoro mwezi wa tatu. Ziara hiyo ya siku tatu waliyoipa
jina la Dom mpaka Moro (bata kwenda bata kurudi) inatarajiwa kufanyika
sehemu mbalilmbali za mkoa wa Morogoro. Akizungumza na Mhariri wa Lukaza
Blog kwa Njia ya Simu Mratibu wa ziara hiyo Mr AMANI KIZUGUTO ameuambia
Mtandao huu ya kwamba taratibu za awali za maandalizi kwa upande mmoja
zimekamilika kwani tayari wameshazungumza na mshauri wa wanafunzi (dean
of students) katika maandalizi ya awali. Alisema wanatarajia katika
ziara hiyo kutembelea mbuga ya wanyama mikumi,maporomoko ya maji katika
milima ya udizungwa huku mazungumzo ya kupitia katika vyuo vikuu
mbalimbali vilivyopo Mkoani Morogoro yakiendelea ili kwenda kufanya nao
matukio mbalimbali ya kijamii.
Pamoja na kujadili mambo ya kielimu. haya sasa kazi kwenu wana udom kwa wale mtakaopenda kwenda wasilianeni na mratibu kwa simu namba
0717 376735
0769 081122

No comments :
Post a Comment