Reward Massawe
Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Kampasi ya Dodoma Bw. Reward Massawe Juzi Tarehe 31/12/2012 saa saba (7) mchana alinusurika kifo masaa machache kabla ya kuuona Mwaka 2013.
Ajali hiyo ilitokea jijini Dar es salaam Eneo la sinza superstar wakati Bw. Reward akiendesha gari aina ya NADIA yenye usajili wa nambari T712 ACR.
Hata hivyo Dodoma universities Corner ilizungumza na Bw. Reward na kutaka kufahamu hasa mazingira ya Ajali hiyo yalikuwaje,Ambapo Reward alisema"Akiwa eneo hilo la sinza superstar (kwenye Mataa) baada ya kuruhusiwa na taa za barabarani Mara ghafla alitokea dereva mmoja wa pikipiki (bodaboda) akiwa amempakia abiria wake na kulazimisha kuchomekea pikipiki yake kwa mbele ya gari hilo kimakosa , hali iliyopelekea Dereva wa pikipiki (Timotheo Martin) kugongwa na kufariki dunia papohapo huku abiria wa pikipiki akiwa ameumizwa vibaya sana"
Kufuatia tukio hilo Tayari taratibu za ki-usalama zilichukua mkondo wake kwa lengo la kufanya uchunguzi na mazingira ya kutokea kwa ajali hiyo.Ingawa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kosa lilikuwa ni la Marehemu Timotheo ambaye alichomekea pikipki yake mbele ya gari alilokuwa akiendesha Bw. Reward.
"Hakika nimeamini na ntazidi kuamini Siku zote kwamba Ajali haina kinga,Sikukutegemea kama hali hii ingetokea.Naamini halikuwa kusudio langu kwa hali hii kutokea, kwani hata mimi nimenusurika katika ajali hii.Hiki ni kipindi kigumu kwangu nahitaji maombi yenu . Maana sio jambo jepesi hata kidogo unaposhuhudia mwenzako akifariki dunia hata kama hukukusudia hali hiyo itokee.Kwa sasa Polisi wanaendelea na kazi yao nadhani hatima ya suala hili itafahamika" Aisema Bw. Reward.
No comments :
Post a Comment