![]() |
ALIYEKUWA RAISI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII ,SANAA NA LUGHA (UDOM) BW. IDD MOHAMEDSiku chache baada ya Aliyekuwa Rais wa Kitivo cha Sanaa ya Jamii, Sanaa na Lugha (UDOM) Kutuhumiwa kwa kufanya ubadhilifu wa kiasi cha Milioni 15.6 mali ya Wanafunzi wa chuo hicho.Hali hiyo imegeuka fundisho kwa vyuo mbalimbali hapa nchini. Akizungumza kwa Masharti ya kutotaja jina lake Mwanafunzi mmoja wa chuo cha St .John amesema mara nyingi viongozi wengi wa serikali za wanafunzi wamekuwa wakijikita katika hali ya kuzitumia fedha za wanafunzi kinyume na taratibu na kutumia fedha kwa lengo la kujinufaisha wenyewe.Katika hatua nyingine kitendo hicho pia kimepelekea Viongozi mbalimbali wa serikali za wanafunzi kujitathmini na kupitia upya hesabu zao hili kuepuka kukumbwa na kashfa za ubadhilifu wa fedha.Kwa upande mwingine kitendo cha Rais wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii ,Sanaa na Lugha Bw. Idd kutiwa nguvuni kimeibua hisia kali kwa wanavyuo walio wengi na wengi wao kuanza kuwa na mawazo ya kuhoji mapato na matumizi ya Fedha zao kwa mujibu wa katiba za vyuo mbalimbali. |
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

No comments :
Post a Comment