![]() |
Bunge la Serikali ya Wanafunzi wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha (UDOM) jana Majira ya Saa Kumi Jioni lilikaa na kuweza Kutoa uamuzi wa Kumvua Madaraka Rais wa kitivo hicho Bw. Idd Mohammed ambaye pia ni Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 wa Kozi ya Biashara na Akaunti (BCOM Accounting). Hatua hiyo imepelekea Baraza zima la Mawaziri kuvunjwa na kupelekea Spika Wa Bunge Kushikilia Serikali Hiyo Kwa Muda (kikatiba).
Hata hivyo hatua hiyo ya kuvuliwa madaraka kwa Rais huyo imekuja ikiwa ni baada ya Raisi huyo (
Idd Mohamed) na waziri wake wa fedha Ibrahim Matata Kushikiliwa na polisi kwa
tuhuma za wizi wa shilingi milioni 15 na laki 6,mali ya serikali ya wanafunzi
wa kitivo cha sayansi ya jamii,sanaa na lugha cha chuo kikuu cha dodoma (udom),Hata
hivyo taarifa kutoka kwa Josephat Lukaza
wa lukaza blog zilisema kuwa Kufuatia tukio hilo Tayari Idd Mohamed ameshikiliwa na jeshi la polisi
kituo cha polisi UDOM kwa tuhuma za wizi wa fedha kiasi cha shilingi milioni 15
na laki 6 .Baada ya kumatwa juzi siku ya alhamisi akiwa na mwenzake Bw. Ibrahim Matata ambaye pia ni
mwanafunzi wa mwaka wa tatu Bcom accounting na kufikishwa katika kituo hicho cha
polisi walikutwa na kiasi cha shilingi milioni 7
laki 2 na 24 elfu (shilingi 7,224,000 za kitanzania.) Na fedha hizo zilitolewa
kwenye account ya serikali ya wanafunzi kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha
na kupelekwa katika akaunti ya mtu binafsi ambaye ni waziri wa fedha Bw.
Ibrahim Matata.
MTUHUMIWA WAZIRI WA FEDHA MATATA IBRAHIM
Raisi
huyo pamoja na waziri wake wa fedha Licha ya kukamatwa juzi na kulala katika kituo cha polisi cha UDOM, Jana Majira ya Saa Moja Jioni Waliweza kuachiwa kwa Dhamana .
Habari zaidi kutoka chanzo chetu cha habari zinasema huenda raisi huyo pamoja na waziri wake wa fedha wakafikishwa mahakamani jumatatu kwa tuhuma za wizi huo. Chanzo Chetu kiliendelea kudai kuwa Kuna fununu zilizozagaa kwa baadhi ya wanafunzi wachache wa kitivo hicho Kuwa Inasemekana Aliyekuwa Raisi Wa Kitivo Hicho ana kashfa ya Kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni Moja laki moja na hamsini elfu ( 1,150,000 ) katika Duka lililopo bweni namba 13 (block 13) ambapo chanzo hicho kimeongeza na kuserma kuwa kulikuwa na ushahidi wa Sauti ambao ulirekodiwa wakati Mtuhumiwa huyo akiomba rushwa kabla ya kukamatwa hapo juzi kwa tuhuma za Wizi wa Shilingi Milioni 15.6 akiwa na aliyekuwa waziri wake wa fedha Ibrahim Matata |
Saturday, January 5, 2013
KUFUATIA UFISADI WA MILLIONI 15.6 ,RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI UDOM KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII SANAA NA LUGHA BW. IDDY MOHAMED AVULIWA MADARAKA YAKE.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

No comments :
Post a Comment