Mwanachuo wa Chuo Kikuu cha St. John
kilichopo Dodoma amekutwa amefariki maeneo ya kikuyu usiku wa kuamkia leo.
Mwanafunzi huyo (mwanamke) anayekadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 50-52 ambaye pia inasemekana alikuwa anasoma shahada ya kwanza ya unesi( Bachelor Degree in Nursing) mwaka wa tatu, Jana mnamo mishale ya saa 3 usiku wakati akitoka kujisomea na wenzake (kwenye discussion) alipokuwa akirejea nyumbani kwake (eneo lililopo karibu na chuo hicho) alikutana na watu wanaosemekana kuwa ni vibaka, ambao walimdhuru na kupelekea kifo chake. Hata hivyo Dodoma universities Corner inafatilia kwa ukaribu sana ili kubaini hasa chanzo kilichopelekea kifo cha Mwanachuo huyo.
Ingawa chanzo chetu cha habari kimebaini kuwa mwili wa marehemu (Mwanachuo huyo) ulikutwa mapema Alfajiri ya leo katika maeneo ya chuo hicho, ambapo mbali na kufariki dunia baadhi ya viungo vya mwili wake vilionekana kuharibiwa vibaya na wanyama wanaodhaniwa kuwa ni fisi.
Tayari taratibu zaidi zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa mwili huo na kupisha uchunguzi wa wa jeshi la polisi juu ya chanzo kilichopelekea kifo cha mwanafunzi huyo.
Dodoma universities Corner itaendelea kuwaletetea habari kamili juu ya kifo cha mwanafunzi huyo....
No comments :
Post a Comment