kuza biashara yako

kuza biashara yako

Pages

Thursday, January 10, 2013

WANACHUO WAFANYA MGOMO, NI BAADA YA WANAFUNZI 54 KU-DISCO,WASEMA HAKI HAIKUTENDEKA,MWENYEKITI WA BODI ANENA...

   Rais  wa Chuo  cha Madini -  Mathias   Kamela

Wanafunzi wapatao  154  wa chuo cha Madini  jumatatu tarehe 07/01/2013   waligoma  kufanya mitihani  ya Supplementary  baada ya  wenzao  55  kusemekana kwamba wali Disco katika mitihani yao. 
Hatua hii ilifikiwa ikiwa inaonekana kuwa historia ya chuo hicho  tangu kuanzishwa kwake  haijawahi kutokea wanafunzi  katika idadi hiyo   Ku- Disco hali ambayo ilionyesha uwepo wa mazingira  ya  kutotendewa haki kwa wanafunzi hao.
Kufuatia  Mgomo huo Dodoma Universities Corner ili zungumza na  Rais wa serikali ya Wanafunzi Bw, Mathias Kamela  ambaye kwa upande wake  kwanza alianza kwa kukanusha kwamba ni Mgomo, akaendelea kwa kusema  " Kilichofanyika sio Mgomo  ila  tulikaa sisi kama serikali ya Wanafunzi kujadili hatua ya  Mazingira  ya kitaaluma ambayo  kimsingi yamekuwa sio rafiki kwetu  (wanachuo)  na kisha tukajaribu kukaa na Management  kujadili matatizo hayo  lakini  mpaka mwisho hatukuweza kufikia muafaka   ndipo  tuliamua  kusitisha zoezi la kufanya  mitihani ya Supplementary kwa Baadhi ya wanafunzi chuoni hapa , Hata hivyo tuliamini maamuzi hayo ni sahihi kwa kuhofia hata  hao walio kuwa wanaingia  kufanya supp  wangeweza kudisco   pia  kutokana  na mazingira ya mitihani ambayo imekuwa ikitungwa ,Mfano  Mwalimu anayefundisha ni tofauti na yule anayetunga Mitihani , hivyo hali  hii  inapunguza  nia  ya mwanafunzi kusoma na kumnyima haki ya msingi   ya  kutimiza kile kilicho mleta hapa chuoni" Alisema  Rais huyo.

Hata  hivyo ikumbukwe kwamba  Chuo cha madini kilifungwa  Tarehe 13/12/2012  baada ya mitihani kumalizika   na kutoa fursa kwa wanachuo hao kwenda likizo  kwa mategemeo ya kurejea  chuoni (kufungua chuo) tarehe  12/01/2013. Kufuatia mlolongo huo baada ya matokeo kutoka wanafunzi  walitakiwa  kufanya mitihani ya supp  tarehe  07/01/2013  mpaka  11/01/2013. 
Baada ya  tarehe   07/01/2013  wanafunzi  kugoma kufanya mitihani ya Supp   waliomba  kukutana na  Mwenyekiti wa Bodi ya chuo hicho  Prof. Mruma, Ambaye alikuja na kukutana na wanafunzi hao  kisha  kukutana  na management   ambapo maamuzi yaliyofikiwa  ilikuwa ni  kufanya uchunguzi  dhidi ya Madai ya msingi ya wanachuo hao ,hatua iliyopelekea  tarehe ya kufungua chuo kusogezwa mbele mpaka   tarehe  29/01/2013  ambapo  kuna uwezekano wa Mitihani ya supp kuanza tarehe  20/01/2013  mpaka  25/01/2013 baada ya uchunguzi wa madai ya wanafunzi kukamilika mpaka itakapofikia tarehe 14/01/2013 imefahamika.
Hata hivyo katika hatua nyingine raisi wa Serikali ya wanafunzi (MRISO)  Bw. Mathias  ameongeza kwa kusema  tatizo sio wanafunzi ku-disco au kupata  supp  , suala  la msingi hapa  ni  kuangalia je  huyo mwanafunzi  alistahili kupata hiyo supp au ku- Disco?  Sasa hapa lazima haki itendeke  kwa  mwanafunzi . Alisema Bw. Mathias.  Alipotakiwa kueleza   nini hasa ambacho kinafanyiwa uchunguzi   mpaka sasa  , Rais huyo  alisema    "Nadhani  wanazo taratibu zao za kuhakikisha  wanakidhi madai yetu ingawa naamini  watapitia mitihani  upya,Mitaala ya chuo  na mambo mengine ambayo wao watadhani ni sahihi kwa lengo la kubaini kasoro"

Mwanafunzi mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake  amesema  kwa hakika yamekuwepo mazingira kandamizi  dhidi yao," Nasikitika baada ya baadhi ya walimu kufikiri  jinsi gani  watuinue kitaaluma wao wanafikiri jinsi  ya kutuangamiza, alisema  Mwanafunzi huyo huku akitokwa na  machozi...

Dodoma Universities Corner inaendelea kufuatilia kwa karibu kwa kila kitakacho kuwa kikiendelea juu ya suala hilo.


No comments :

Post a Comment