kuza biashara yako

kuza biashara yako

Pages

Monday, January 7, 2013

HUYU NDIYE JOSEPHAT MUSHI,MWANACHUO ALIYEHITIMU CHUO CHA MADINI 2011- MWENYE NDOTO YA KUJIAJIRI.

Photo: hapa kazi tu ..
 Josephat Mushi

Josephat Mushi  ni miongoni  Mwa Wanafunzi walio wahi kusoma chuo cha Madini Dodoma na Alihitimu   Mwaka 2011  akiwa na  Diploma ya Geology  and Mineral Exploration. Kijana huyu ni miongoni mwa Vijana wachache ambao wamekuwa na mitazamo   ya Kujiajiri  zaidi kuliko kuajiliwa. Kwa sasa anafanya kazi katika kampuni ya African Barrick Gold - Nyamongo ,Mara,Tanzania  yeye ni  geo tech ( ambaye  hasa anashughulikia  ku- control Gold  Grade)

Bw. Josephat anakuja na mtazamo ufuatao kwa wanachuo wenzake waliosoma madini lakini analeta  changamoto kwa wanavyuo wengine  wenye taaluma mbalimbali. 
HUU NI MUDA WETU WA KUJIAJIRI KW TAALUMA ZETU TULIZONAZO NA KUACHWA KUAJIRIWA
Guys wana madini tunaoitwa kada ya kati...chuo kinazidi kutapika vijana na ajira migodini zina zidi kubana maana kila kukicha wageni wenye elimu kiduchu kuliko ya kwetu sisi wanapewa kipaumbele na kulipwa mabilioni lukuki na sisi tukibakiwa na faranga za kubadili nguo na kusogeza siku baaada ya kukaa na kutafakari na baadhi ya wdau ambao nao wanamtizamo wa mihangaiko kama mimi tukaja na wazo moja ambalo nafikiri kwa kupitia taaluma tulionayo tunaweza jikuta tunakwenda kwa wazungu kuchukua  uzoefu  na kimtaji kidogo tu....wazo lenyewe naweza liita hivi
MADINI MINING GROUP...Ambapo hizi ni group zitakazo undwa na wataalamu wajiologia,mainjinia na wachenjua,wasiozidi kumi kwa ratio ya 3;3;4 kila kozi angalau wenye uzoefu usiopungua mwaka mmoja kadi migodi tofauti

MAKUNDI HAYA YATAFANYA NINI??????
KWANZA yataanza kwa kuchanganya kamtaji kadogo kama mil 10 ambazo watanunua baadhi ya vifaa kama crushers na vingine vya kitaalamu na vile visivyo muhimu sana wanaweza kukodi
 
WATAFANYA NINI????
Hawa kwa umoja wao watashirikiana na wachimbajiwadogo wadogo waliozagaa tz nzima ,chunya,nzuguni,kanda ya ziwa kote katika swala zima la kure cover dhahabu na madini yote,wanaweza hata kuanza kw kusaga tailings zilizoachwa na wachimbaji wadogo wdogo ..GEOLOGY WATAKUWA WAKITUMIA TAALUMA YAO KUWADIRECT SMALL MINERS SEHEMU YENYE POTNTIAL NA KUPATA madini kwa urahisi, wahandisi watasaidi katika kuwaelimisha hawa wachimbaji namna ya kuchimba mashimo yenye usalama ..hii ni kwa kifupi ila najaribu kuwapa mwanga ambao mimi na BW kunju (wanafanya kazi wote na walisoma wote pia) tuliweza kuugundua tulipokuwa tumeekaa pit tuna spot ore ya mzungu

jinsi tunavyokuwa tutanunua dhahabu na madini ya wachimbaji wadogo na mwisho wa siku madini ya dodoma itakuwa zaidi ya sasa maana tunadharaulika na haijulikana tumesomea wapi ....kama unafkiri tunaweza shirkiana join me. 
 
Anapatikana kwa simu namba  0713795928  kuanzia saa 2 usiku hadi saa3 usiku kila siku na jumatatu siku nzima...

STRIVING FOR BETTER FUTURE GUYZ

No comments :

Post a Comment