Hivi karibuni Kamera yetu Imemnasa mwanachuo mmoja wa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) akiwa katika dimbwi la Mawazo , hali ambayo siyo ya kawaida saaana , Hata hivyo haikufahamika mara moja kwamba mwanachuo huyo alikuwa anawaza nini muda huo.
Katika kutaka kujua kile kilichokuwa kikiendelea na kumsonga mwanachuo huyo,Dodoma universities corner ilijaribu kuzungumza na Mwanachuo huyo kujua nini hasa kilikuwa kinamkabili muda huo, hata hivyo hakuwa tayari kuzungumza lolote.
Wakati mwingine Wanachuo hukumbana na Misongo ya mawazo ambayo mara nyingi husababishwa na Matatizo ya kifamilia, Mahusiano baina yao wawapo chuoni, Masomo na mambo mengine mengi ambayo yanaweza kumkuta binadamu yeyote Duniani.
Ingawa sio wote wanao onekana kwamba wana mawazo huwa kweli wana waza/au kuwa na msongo wa mawazo, wakati mwingine ni kile kinacho fahamika kama "Mapozi"

No comments :
Post a Comment