JESHI la
polisi mkoani Dodoma limeshutumiwa kwa kushindwa kuimarisha ulinzi
katika baadhi ya maeneo mkoani humo hatua inayodaiwa kuchangia kuaawa
kinyama kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Saint John
Mwanafunzi huyo wa uuguzi katika chuo Kikuu cha St. John
kilichopo mkoani Dodoma na ambaye alikuwa muuguzi katika hospitali ya
Kilimatinde, Manyoni, Singida Kufariki dunia baada ya kubakwa na kisha kuuawa
na watu wasiojulikana.
Hata hivyo,Mwili wa marehemu
huyo aliyetambuliwa kwa majina Lyidia Mzima mwenye umri wa miaka
57, ulikutwa umetupwa kichakani na tayari ulishaliwa na fisi.
Inataarifiwa kuwa marehemu alipatwa na masaibu hayo alipokuwa ametoka kujisomea, akiwa anarudi anakoishi katika nyumba ya kupanga, Kibaoni-Image B, katika kata ya Kikuyu Kusini, iliyopo karibu na chuo hicho.

Kamanda wa Polisi
mkoa wa Dodoma, David Misime amethibitisha kutokea kwa tukio hilo juzi usiku na
kwamba marehemu alionekana kunyofolewa nyama za mapajani.
Kutokana na shutuma za uzembe dhidi ya jeshi hilo, Kamanda wa mkoa ACP David Misime anawataka wakazi wa mkoa huo kuimarisha ulinzi shirikishi kwa lengo la kuwabaini wahalifu.
Wakati huo huo Kamanda Misime anasema msako mkali umeanza wa kuwatia nguvuni waliohusika na ukatili huo ili waweze kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwa ajili ya hukumu. Kiongozi wa wanafunzi wa chuo hicho aliongeza kuwa aliuona mwili wa marehemu ukiwa umechunika ngozi kuanzia utosini hadi sehemu ya kisogoni.
Mwili wa marehemu
uligunduliwa na wananchi ambao walisema kwa siku mbili ilikuwa ikisikika milio
ya sauti za fisi kutoka katika eneo ambapo mwili wa marehemu ulikutwa.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Dodoma ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Dodoma ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Makamu Mkuu wa Chuo
hicho, Profesa Gabriel Mwaluko alithibitisha tukio hilo na kusema hayo yote
yanatokana na chuo kukosa mabweni ya wanafunzi kulala jambo ambalo linafanya
wanafunzi wengi kwenda kupanga mitaani na kukumbwa na matukio mbalimbali.
Mei mwaka jana, wanafunzi wa chuo hicho waligoma kuingia madarasani hadi wawasilishe malalamiko yao kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kupigwa nondo, kuibiwa vitu kulawitiwa na hata kubakwa. Walisema sababu nyingine inayochochea matukio hayo ni chuo kukosa uzio na hivyo kurahisisha mwingiliano wa watu na wanachuo.

Hivi karibuni
wanachuo wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dar es Salaam waliandamana
wakipinga kukithiri kwa vitendo vya wizi, ubakaji na ulawiti katika hosteli zao
zilizoko Kigamboni

No comments :
Post a Comment