Bonajesuit
Rischard
Katika Maisha yake Bonajesuit
Rischard atayakumbuka mengi lakini zaidi ni kuhusu safari yake ndefu ya kimasomo akiwa katika Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)
" Mwaka 2012 ni mwaka ambao watu mbalimbali waliweza kutimiza ndoto zao,lakini kwa upande wake anafurahi kuweza kuhitimu elimu yake katika ngazi ya Shahada (Shahada ya kwanza) ya biashara na uhasibu.
Waswahili wanamsemo flani wanasema "kazi sio kufanya kazi bali kazi ni kutafuta kazi/kupata kazi" kauli hii inakuwa na maana kubwa hasa katika kizazi hiki cha sasa ambapo ongezeko la wasomi ni kubwa sana ukilinganisha na fursa za ajira zilizopo.
Sasa anayomatumaini mapya baada ya kufanikiwa kupata kazi, Anasema " Vijana wengi tunapenda kujiajiri lakini kimsingi tunakwamishwa na ukosefu wa mitaji licha ya kuwa na uelewa wa taaluma mbalimbali za kibiashara (ujasiriamali) ,hivyo inatulazimu kutafuta mahali pa kufanya kazi ili mwisho wa siku tuweze kupata kianzio cha mtaji. Ingawa bado ajira nazo ni changamoto kubwa, Hivyo na mshukuru Mungu kupata mahali pa kufanya kazi kwa sasa" Alisema Bonajesuit.
Hata hivyo ,anaongeza kwa kusema Taaluma aliyoipata UDOM ndiyo ilimuwezesha yeye kupata ajira aliyo nayo sasa licha ya ushindani mkubwa aliokuwa nao dhidi ya wenzake wakati wa usahili,Hivyo anadiriki kusema "Hatua ya yeye kupata Kazi ni kwa Msaada mkubwa wa Chuo Kikuu Cha Dodoma"
Bonajesuit (wa pili kutoka kulia ) akiwa na wahitimu wenzake katika mahafali ya tatu ya Chuo kikuu cha Dodoma


No comments :
Post a Comment