Baadhi ya Wanafunzi wa CBE -Dodoma ( Picha na Maktaba yetu)
Wanafunzi wa CBE wameibuka na kusema kwamba wao pia wanaliomba jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi katika maeneo ya Chuo hicho. Akizungumza na Dodoma Universities Corner Mwanafunzi mmoja wa Chuo hicho aiyejitambulisha kwa jina mmoja la Mackson, Amesema wakati umefika kwa Jeshi la polisi kuimarisha ulinzi kwa vyuo vyote ikiwemo chuo hicho (CBE). "Wanafunzi wa chuo chetu kwa ujumla wake wanakadiliwa kufikia 5000 hii ni idadi kubwa , Hostel za chuo chetu hazitoshelezi kwa idadi hiyo ,hivyo wanafunzi tunalazimika kupanga maeneo yaliyoko nje ya chuo. Mfano wanafunzi wengi wamepanga maeneo ya Airport, Railway , Makole ,Area A,Area D ,Area E, Ipagala, Chadulu,Mlezi,Kikuyu na wengine wamepanga maeneo ya Nkuhungu. Sasa fikilia sasa hivi tunaelekea kwenye mitihani ya Semester ya kwanza kwa wanafunzi wa Diploma II na Bachelor Degree, kufuatia hali hii wanafunzi wengi huwa tunajisomea hapa chuoni kupitia Discussion mpaka mida ya saa tano /saa sita , Kwa hali hii ulinzi unahitajika kwani wakati mwingine baadhi ya wanafunzi tunahofia vitisho wakati wa kurudi katika makazi yetu, ndio maana naona umuhimu wa jeshi la polisi kuimarisha ulinzi" Alisema Mwanafunzi huyo.
Tusisubiri mpaka matatizo yatokee ndio tuamue kuchukua hatua ,Hatua zinatakiwa kuchukuliwa kuanzia sasa..Alisema Bw.Mackson
Hali hii ya wanafunzi kujawa na hofu inakuja ikiwa ni siku chache tangu kuaawa kwa mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha St.John mkoani Dodoma na kufuatiwa vitendo vya uvamizi kwa wanafunzi kwa kuporwa Laptop na simu zao.Licha ya matukio kama haya kutokea pia kwa wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wiki chache zilizopita.

No comments :
Post a Comment