Thursday, January 31, 2013
Monday, January 28, 2013
TASWIRA YA "MBONI SHOW " ILIYOHUSISHA WANAVYUO WA DODOMA
Wanachuo wa CBE wakielekea Dodoma Hotel kushiriki katika kipindi cha Mboni Show.
Timu ya Mboni Show jana ilikuwa mkoani Dodoma katika Hotel ya Dodoma (Dodoma Hotel) kwa kuwakutanisha Baadhi ya Wanavyuo kutoka vyuo mbalimbali vya Hapa Dodoma. Hata hivyo mada kubwa iliyojadiliwa ilikuwa ni kuhusu MA- SUGAR DADIES DHIDI YA VIJANA WA KIKE " Mada hiyo ilitoa fursa kwa wanavyuo hao kuchangia kwa kina sababu ambazo hupelekea akina dada hususani wale wenye umri mdogo na wale wa vyuoni kushiriki katika vitendo vya ngono.
Muonekano wa Baadhi ya wanachuo mara baad ya Kuwasili Dodoma Hotel
Jamani Tumetokelezeaaa....
Mada ilikuwa safi ....
Wakisikiliza kwa makini kile kilichouwa kinaendelea...
Sasa mambo ya meanza....
Majadiliano yakiendelea ....
Saturday, January 26, 2013
CBE WANENA "NA SISI TUNAHITAJI ULINZI" ...
Baadhi ya Wanafunzi wa CBE -Dodoma ( Picha na Maktaba yetu)
Wanafunzi wa CBE wameibuka na kusema kwamba wao pia wanaliomba jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi katika maeneo ya Chuo hicho. Akizungumza na Dodoma Universities Corner Mwanafunzi mmoja wa Chuo hicho aiyejitambulisha kwa jina mmoja la Mackson, Amesema wakati umefika kwa Jeshi la polisi kuimarisha ulinzi kwa vyuo vyote ikiwemo chuo hicho (CBE). "Wanafunzi wa chuo chetu kwa ujumla wake wanakadiliwa kufikia 5000 hii ni idadi kubwa , Hostel za chuo chetu hazitoshelezi kwa idadi hiyo ,hivyo wanafunzi tunalazimika kupanga maeneo yaliyoko nje ya chuo. Mfano wanafunzi wengi wamepanga maeneo ya Airport, Railway , Makole ,Area A,Area D ,Area E, Ipagala, Chadulu,Mlezi,Kikuyu na wengine wamepanga maeneo ya Nkuhungu. Sasa fikilia sasa hivi tunaelekea kwenye mitihani ya Semester ya kwanza kwa wanafunzi wa Diploma II na Bachelor Degree, kufuatia hali hii wanafunzi wengi huwa tunajisomea hapa chuoni kupitia Discussion mpaka mida ya saa tano /saa sita , Kwa hali hii ulinzi unahitajika kwani wakati mwingine baadhi ya wanafunzi tunahofia vitisho wakati wa kurudi katika makazi yetu, ndio maana naona umuhimu wa jeshi la polisi kuimarisha ulinzi" Alisema Mwanafunzi huyo.
Tusisubiri mpaka matatizo yatokee ndio tuamue kuchukua hatua ,Hatua zinatakiwa kuchukuliwa kuanzia sasa..Alisema Bw.Mackson
Hali hii ya wanafunzi kujawa na hofu inakuja ikiwa ni siku chache tangu kuaawa kwa mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha St.John mkoani Dodoma na kufuatiwa vitendo vya uvamizi kwa wanafunzi kwa kuporwa Laptop na simu zao.Licha ya matukio kama haya kutokea pia kwa wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wiki chache zilizopita.
WANAFUNZI UDOM WAPANGA KUFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO MKOANI MOROGORO MWEZI WA TATU
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wamepanga kufanya ziara ya kihistoria mkoani Morogoro mwezi wa tatu. Ziara hiyo ya siku tatu waliyoipa
jina la Dom mpaka Moro (bata kwenda bata kurudi) inatarajiwa kufanyika
sehemu mbalilmbali za mkoa wa Morogoro. Akizungumza na Mhariri wa Lukaza
Blog kwa Njia ya Simu Mratibu wa ziara hiyo Mr AMANI KIZUGUTO ameuambia
Mtandao huu ya kwamba taratibu za awali za maandalizi kwa upande mmoja
zimekamilika kwani tayari wameshazungumza na mshauri wa wanafunzi (dean
of students) katika maandalizi ya awali. Alisema wanatarajia katika
ziara hiyo kutembelea mbuga ya wanyama mikumi,maporomoko ya maji katika
milima ya udizungwa huku mazungumzo ya kupitia katika vyuo vikuu
mbalimbali vilivyopo Mkoani Morogoro yakiendelea ili kwenda kufanya nao
matukio mbalimbali ya kijamii.
Pamoja na kujadili mambo ya kielimu. haya sasa kazi kwenu wana udom kwa wale mtakaopenda kwenda wasilianeni na mratibu kwa simu namba
0717 376735
0769 081122
Friday, January 25, 2013
"A" TO " Z" YA MAANDAMANO YALIYOFANYWA JANA NA WANAFUNZI WA ST JOHN MKOANI DODOMA
| ||
| Wanafunzi baada ya kusubili kwa muda mrefu kibari icho wakaamua kuandaa mabango kwa ajili ya maandamano, ambapo kibari kipatikane kisipatikane walidai kuandamana ni lazima |
| Mabango yalipokamilika wakasimama kwenye bendera kwa mara nyingine |
| Walifika mbali na kuona kuwa polisi wanahusika katika mambo mabaya wanayofanyiwa. Ndipo wakachora bango hili kuonyesha hisia zao |
| Hapa wapo barabarani na masomo kwa siku ya leo hayakuwepo |
| Bango lina picha ya mwanafunzi alieuliwa kikatili, aliefahamika kwa jina la Bi.LYDIA |
| Ni mchaka mchaka ulioendana na nyimbo za hisia |
| Haya huyu anaashiria demokrasia na maendelea ndio imetawala juu yao |
| Msafara hapa unaelekea maeneo ya Bungeni |
| Kila walipopita walikuwa wakishindikizwa na polisi kuhakikisha amani inatawala |
| Gari la maji ya kuwasha lilikuwepo lakini wanafunzi hao hawakutishika na kitu chochote kile kutoka kwa Polisi |
| Wanafunzi walifika mpaka Nyerere Square waliimba nyimbo mbalimbali mahala hapo |
| Baada ya kutembea mji mzima na mabango yao na kuhakikisha kiu yao imekwisha basi waliamua kurudi chuoni |
| Gari la washa washa nalo lilikuwepo lakini watu walikuwa na jaziba zao vilevile mwanzo mwisho |
| Barabara zilikuwa zimetawaliwa na wanafunzi kwa kiasi kikubwa, mpaka kusababisha magari kutopita |
| Hapa ndipo safari ya maandamano ilipoanzia na ndipo safari hiyo ilipoishia maeneo haya ya kwenye bendera mbele ya jengo la administration. |
Safari ya maandamano ya amani ikawa
imeishia chuoni hapo baada ya kuona kuwa ujumbe wao umefika. Wanafunzi
wa chuo wamechoshwa na matendo mabaya ambayo wanafanyiwa ikiwa ni pamoja
na kubakwa, kulawitiwa, kuibiwa vitu vyao kama Laptop na vitu vingine.
Wameonesha umoja wao kwa sababu ya kuchoshwa na mambo hayo, ambapo jana
asubuhi kuna wanafunzi walivamiwa na kuibiwa Laptop. Hivyo wakaamua
kujikusanya asubuhi hiyo hiyo mida ya saa kumi na mbili alfajili na
kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye walimpiga na baadae
kuchukuliwa na polisi.
Subscribe to:
Comments
(
Atom
)





