PENGINE haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na
utandawazi. Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika
masomo yao na kazi, lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo.
Uchunguzi wa gazeti la mwananchi hivi karibuni umebaini kuwa matumizi mabaya ya teknolojia
hasa mitandao ya kijamii yamechochea ongezeko la uhalifu, ubakaji,
matumizi ya dawa za kulevya na zaidi biashara ya ukahaba vyuoni.
Mitandao ya ‘Facebook’, ‘Twitter’, ‘BBM’, ‘Instagram’ inafahamika kwa
namna inavyoweza kuwaunganisha watu kutokana na urahisi wake katika
kuitumia.
Gazeti Mwananchi limebaini kuwa katika mitandao hiyo makundi mbalimbali yameanzishwa yakiwa na malengo tofauti.
Baadhi wameanzisha makundi kwa lengo la kujenga mitandao ya
kibishara, kidini, michezo, burudani, vichekesho na mengine ambayo mara
nyingi huwa wazi na yeyote anaweza kujiunga na kuona kinachoendelea
ndani.
Mbali na hayo ndani ya mtandao wa ‘Facebook na ‘BBM’ yapo makundi
yanayoendesha biashara ya ukahaba, yakiwahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu
mbalimbali nchini.
Uchunguzi umebaini kuwa wanafunzi hao wanaofanya biashara ya ukahaba
kwa kutumia mitandao wameweka picha na namba kwa ajili ya mawasiliano
kwa mteja atakayekubaliana na bei waliyoweka.
Baadhi ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania
Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu
Tanzania’ na nyingine katika kufanikisha biashara hiyo ya ngono.
Ukiingia katika mitandao ya Facebook, Twitter, BBM, Instagram,
utabaini kuwapo kwa makundi yaliyoundwa kutengeneza mitandao ya ngono,
ambayo huweka pia namba za simu za wahusika, zikiambatana na picha,
ambao ikiwa utaangalia picha na kuvutiwa, unaweza ukapiga simu husika
kuzungumza naye kwa kufanya mapatano kabla ya kukubaliana.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa mwanamume anaweza
kumpata msichana kutoka chuo kikuu chochote nchini anayefanya biashara
ya ukahaba kupitia mitandao hiyo.
Baadhi ya vyuo wanavyotoka wasichana wanaofanya biashara hiyo na
kujitangaza kwenye mitandao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine
(SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM).
Kwa nyakati tofauti, waandishi wa gazeti hili walitembelea makundi yanayojinadi kufanya biashara hiyo pamoja na kufanya mawasiliano na wasichana watatu ambao waliweka picha na namba zao kwenye mtandao.
Kwa nyakati tofauti, waandishi wa gazeti hili walitembelea makundi yanayojinadi kufanya biashara hiyo pamoja na kufanya mawasiliano na wasichana watatu ambao waliweka picha na namba zao kwenye mtandao.
Wasichana hao walijitambulisha kwa majina, vyuo na vitivo wanavyosoma
na baada ya kuwafuatilia kwa kuweka ahadi za kimapenzi ilithibitika
kuwa wanafanya biashara ya ukahaba huku wakiwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Mmoja wa wasichana hao alijitambulisha kwa jina la Bianca (sio jina
lake halisi), ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili Kitivo cha Sheria,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baada ya mwandishi kufanya naye mawasiliano walikubaliana kukutana
eneo la Udasa na muda wa ahadi ulipofika, mwandishi alifika eneo hilo na
kukutana na binti huyo ambaye aliiona picha yake na namba ya simu
kwenye mtandao, tofauti na alivyodhani awali kuwa huenda wasichana hao
wanatumia picha za watu wengine kujinadi.
Kutokana na lengo la msichana kuwa ni biashara ya ngono, mwandishi wa
gazeti hili alilazimika kumpeleka binti huyo katika hoteli moja maarufu
jijini, akimweleza kuwa inabidi wanywe pombe kwanza kabla ya kwenda
chumbani kwa makubaliano ya kumlipa Sh50,000.
Binti huyo alikabidhiwa fedha hizo ili kumwaminisha uhalisia wa
kuwapo hitaji na muda wa kwenda naye chumbani ulipofika waliongozana
lakini mwandishi akatoroka njiani akiwa amethibitisha kuwapo kwa tabia
hiyo.
Gazeti la Mwananchi lilimfuatilia mwanafunzi mwingine ambaye alijitambulisha
kuwa anasoma katika Chuo cha Ustawi wa Jamii, ambaye kama ilivyokuwa kwa
wa kwanza, hakupata taabu kujieleza.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili baadhi ya wanafunzi walikiri kuwa katika vyuo kuna wasichana wanaojiuza, ingawa walisema kuwa, hawajui kama wamefikia hatua ya kuweka picha katika mitandao na namba za simu.
Baada ya mwandishi kueleza alipoipata namba yake mazungumzo yao yalikuwa hivi:
Binti aliuliza: “…Kwa hiyo, uko wapi?”
Mwandishi alijibu: “Nipo Ubungo.”
Binti akauliza tena: “Unaweza kuja Ustawi?”
Binti aliuliza: “…Kwa hiyo, uko wapi?”
Mwandishi alijibu: “Nipo Ubungo.”
Binti akauliza tena: “Unaweza kuja Ustawi?”
Baada ya mawasiliano hayo mwandishi aliambiwa binti huyo kuwa anaweza kumfuata chuoni hapo.
Mwandishi wa gazeti la mwananchi alifika maeneo ya Kijitonyama
jirani na kilipo chuo hicho, na kumpigia simu binti huyo, ambaye
aliipokea na safari hii alimwambia mwandishi kuwa ikiwezekana aje na
rafiki yake.
Ilichukua nusu saa kwa wasichana hao kufika katika baa, ambayo
mwandishi alikaa kuwasubiri, mara walitokea wasichana hao wakiwa
wachangamfu, warembo waliovalia mavazi ya kisasa, yaliyoacha sehemu
kubwa ya miili yao wazi.
Muda wa dakika saba walizokaa zilitosha kuwafanya wazoeane na
mwandishi kama vile waliwahi kukutana miaka mingi ya nyuma, stori,
vinywaji na mambo yalifanyika kama ilivyokuwa Udasa.
gazeti la mwananchi Jumapili liliendelea na uchunguzi wake kwa
wasichana wengine ambao wameweka picha zao katika mitandao hiyo
wakijiuza, ambapo walipopigiwa simu walijibu na kufika katika maeneo
waliyokubaliana.
Gazeti la mwanachi liliwasiliana na wasichana zaidi ya 10 kutoka
katika vyuo tofauti jijini na wote walikiri kuwa wapo katika biashara
wakieleza kuwa mteja akipatikana wanaweza kukubaliana malipo.
Wasichana hao ni tone kati ya mamia ya wanafunzi wa vyuo, ambao hivi
sasa wamebuni njia hiyo baada ya kuona ule mtindo wa kujiuza nyakati za
usiku katika maeneo mbalimbali kuwa umeanza kupitwa na wakati.
Baadhi ya wasichana wanaofanya biashara hiyo hasa mkoani Dodoma,
wamekuwa wakiwatumia mawakala ambao huwapa namba za simu na pindi
anapotokea mteja, huunganishwa na kiongozi wa kikundi hicho kabla ya
kupata aina ya msichana anayetaka.
Hata hivyo mteja asiporidhika na msichana aliyeletewa, hutafutiwa
mwingine, huku pia wasichana husika wakitofautiana mahitaji kabla ya
kufanya nao ngono.
Wapo wanaoweka masharti ya kunyweshwa pombe kwanza, kupelekwa disko
au kwenye muziki pamoja na wanaokwenda kwa matakwa ya mteja moja kwa
moja.
Wanafunzi wazungumzaWakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili baadhi ya wanafunzi walikiri kuwa katika vyuo kuna wasichana wanaojiuza, ingawa walisema kuwa, hawajui kama wamefikia hatua ya kuweka picha katika mitandao na namba za simu.
Mwanafunzi Aisha Idd wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), alisema
kuwa biashara ya ukahaba inafanyika, lakini hafahamu kama wanatumia
mitandao kujitangaza.
“Sijawahi kufikiria kama wanaweza kufika mbali kiasi hiki, sijui kama
wanajiuza kwenye mitandao, lakini hii inaonyesha kuwa tunakoelekea ni
kubaya zaidi kwani hawa ndio watu wanaotegemewa katika ujenzi wa taifa,”
anasema Aisha na kuongeza:
“Ninafikiri Serikali inapaswa kuliangalia hili, yaani wasomi ndiyo
wanaoongoza kwa kufanya mambo machafu, hii ni aibu na inaweza kuitia
doa sekta nzima ya elimu ionekane haina maana kama msomi wa chuo kikuu
anaweza kufanya upuuzi huu.”
Naye John Mkongo alisema kuwa hashangai kusikia kuwa wanafunzi hao
wametafuta njia nyingine ya kutafutia wateja kwa kuwa wanaweza kufanya
chochote ili wapate pesa za kufanyia starehe.
“Hii inawezekana kabisa kwani hawa dada zetu wamefikia kufanya mambo
ya ajabu kama vile wamepata wazimu, ili kupata pesa wanaweza kukubali
kufanya chochote, najua siku za usoni tutaendelea kusikia mambo ya ajabu
zaidi kwani hawa wenzetu wamejitoa mhanga,” anasema Mkongo.
Anaongeza kuwa kinachowafanya wasichana hao kujiingiza katika
biashara ya ukahaba ni tamaa, akitoa mfano baadhi ya wasichana ambao
hawajihusishi kabisa na mambo hayo.Mimi ninaona kinachowagharimu hawa
dada zetu ni tamaa tu, huku wengine wakiponzwa na ulimbukeni wa kuvamia
mambo, ambayo wameanza kuyaona baada ya kuingia chuoni hasa kupenda vitu
vya gharama kama vile simu, nguo, manukato na magari,”anasema Mkongo.
Wakuu wa vyuo wanena
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Tolly Mbwete anasema hali hiyo inatokana na kukua kwa utandawazi.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Tolly Mbwete anasema hali hiyo inatokana na kukua kwa utandawazi.
“Ni wakati sasa kwa wizara inayohusika (Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo ) kuhakikisha inafuatilia jambo hili na kuchukua
hatua stahiki,” anasema Profesa Mbwete na kuongeza:
“Elimu nayo inatakiwa kutolewa kwa watumiaji ili kutokuathiri dhamira ya kukua kwa utandawazi, jamii nzima ielimishwe kuhusu matumizi sahihi ya mitandao hiyo.”
hasa wanapofika vyuoni na kwamba hawataki kukaripiwa au kuonywa.
“Akiwa nyumbani anakuwa mtaratibu lakini akitega mgongo kutoka kutoka nyumbani anaanza tena ujinga wake, hivyo kama vitendo hivyo vipo basi Serikali inatakiwa kufuatilia na kuchukua hatua zaidi,”anasema
source mwananchi
“Elimu nayo inatakiwa kutolewa kwa watumiaji ili kutokuathiri dhamira ya kukua kwa utandawazi, jamii nzima ielimishwe kuhusu matumizi sahihi ya mitandao hiyo.”
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Idris Kikula,
anasema kuwa hana taarifa za kuwapo kwa makundi hayo lakini akabainisha
kuwa unatakiwa kuwapo kwa utafiti ili kujiridhisha kama ni kweli hao
wanaofanya hivyo ni wanafunzi wa vyuo.
Anasema kama yapo ni wakati sasa wa kuhakikisha wanakemewa kwani kuna
baadhi ya wasichana wanatumia mitandao kujitambulisha kuwa ni wanafunzi
wa vyuo, wakati siyo wanafunzi.
“Hapa Dodoma katika kipindi cha Bunge wanawake wanaojiuza huwa wengi
kila unayemuuliza atakwambia anasoma chuo, lakini ukimuuliza kozi gani
atakwambia bado sijapangiwa hivyo hii ni hatari,” anasema Profesa
Kikula.
Wazazi wasikitika
Mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, Florence Baltazar anasema vitendo hivyo vinatokea kwa sababu ya kuiga mambo ya nchi za nje.
Mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, Florence Baltazar anasema vitendo hivyo vinatokea kwa sababu ya kuiga mambo ya nchi za nje.
Baltazari anasema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), inatakiwa
kuhakikisha inafuatilia mitandao hiyo ikibidi kuifunga kabisa.
Zubeda Hamza anasema vijana wa siku hizi hawajitambui hususan wasichana ambao wamekuwa hawapo makini na utu wao.
Zubeda Hamza anasema vijana wa siku hizi hawajitambui hususan wasichana ambao wamekuwa hawapo makini na utu wao.
“Kweli kama msichana anajitambua hawezi kutongozwa katika mtandao na
kukubali haraka au kujinadi hivyo wasichana wanatakiwa kutambua utu
wao,”anasema na kuongeza:
“TCRA inatakiwa kuwa inafanya mapitio ya mitandao yote ili ile inayokiuka taratibu waweze kuifungia.”
Kwa upande wake Charles Mashiri anasema kuwa wasichana wa siku hizi wamekuwa hawashikiki,hasa wanapofika vyuoni na kwamba hawataki kukaripiwa au kuonywa.
“Akiwa nyumbani anakuwa mtaratibu lakini akitega mgongo kutoka kutoka nyumbani anaanza tena ujinga wake, hivyo kama vitendo hivyo vipo basi Serikali inatakiwa kufuatilia na kuchukua hatua zaidi,”anasema
source mwananchi
No comments :
Post a Comment