HUYU NDIYE MWANAFUNZI WA CBE ALIYEFARIKI DUNIA TAREHE 08/02/2013
Marehemu Baraka Luhizo (Msomali)
Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Kampasi ya Dodoma Bw. Baraka Luhizo ali - maarufu kama MSOMALI Alifariki dunia siku ya Ijumaa wiki iliyopita (Tarehe 08/02/2013 ) Tuliani - morogoro.
Kwa mujibu wa Chanzo chetu cha Habari , Marehemu alikutwa na Mauti hayo baada ya kudondokewa na Mwamba hali iliyo sababisha kufariki dunia. Hata hivyo Mwili wa marehemu ulizikwa Tarehe 09/02/2013 baada ya mwili huo kuharibika vibaya.
Marehemu Baraka Luhuzo (Msomali) ,Alikutwa na Mauti hayo ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu ahitimu Elimu yake katika ngazi ya Diploma (Diploma in Business Administration) katika chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma.
BAADHI YA PICHA MBALIMBALI ZINAZO MUONYESHA MAREHEMU BARAKA ENZI ZA UHAI WAKE...

Picha ya juu: Marehemu Baraka kulia akiwa na Moja ya Marafiki zake, Enzi za uhai wake
No comments :
Post a Comment