kuza biashara yako

kuza biashara yako

Pages

Sunday, June 8, 2014

HIKI NDICHO ALICHO KIFANYA DIAMOND!!!!! KATIKA TUZO ZA MTV

Hongera sana Diamond kwa ulipofkia, sio pabaya hata kidogo. Jipange next tym utafanya vema sana. Watanzania  tuhamishieni nguvu kwenye Tuzo nyingine kama Kora, na BET. Tumuwezeshe huyu kijana wa Kitanzania.

Thursday, June 5, 2014

PINDA ATEMBELEA SHULE YA WASIOONA YA BIGIRI CHAMWINO– DODOMA

PG4A1456Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama  baadhi ya michoro unayotumika katika kuwafundishia  wanafunzi wasiona  wakati alipotombelea shule maalu ya Wasioona ya Bigiri Dodoma Juni4,2014. Kulia ni Mratibu wa Mpango wa kuifadhili shule hiyo, Bw. V. Ramadhar Reddy  ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  SURA. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A1467Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama  baadhi ya michoro unayotumika katika kuwafundishia  wanafunzi wasiona  wakati alipotombelea shule maalu ya Wasioona ya Bigiri Dodoma Juni4,2014. Kulia ni Mratibu wa Mpango wa kuifadhili shule hiyo, Bw. V. Ramadhar Reddy  ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  SURA. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PG4A1493Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua majengo na vifaa vya  kufundishia  wakati alipotembelea Shule Maalu ya Wasioona ya Bigiri iliyopo Dodoma Juni 4, 2014 Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Reheme Nchimbi Juni 4, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A1512Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na walimu,  baadhi ya wanafunzi na watendaji wa  wilaya ya Chamwino wakati alipotembelea   shule ya wasiiona ya  Bigiri  Juni 4, 2014, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi na kulia ni Mratibu wa Mpango wa kuifadhili shule hiyo, Bw. V. Ramadhar Reddy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Sunday, June 1, 2014

VIJANA WAASWA KUJIEPUSHA NA NDOA KATIKA UMRI MDOGO

PIX 3 (2)
Afisa Msaidizi wa Vijana kituo cha UMATI tawi la Dar es Salaam Bi. Upendo Daud akiwaeleza vijana kuhusu mada kuu ya Tamasha ambayo ni “Athari za ndoa za utotoni” wakati wa ufunguzi wa tamasha la mwezi katika kituo hicho.

PIX 5 (1)Mwenyekiti wa mtaa wa Wailes Bw. Abdul Kidege ambaye ndiye mgeni rasmi katika Tamasha la Jamvi la vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam akitoa hotuba yake fupi kwa vijana waliohudhuria tamasha hilo lenye lengo la kuwaeleimisha vijana juu ya athari za ndoa za utotoni.
PIX 6 (1)PIX 7Vijana wakifuatilia kwa makini hotuba ikiyotolewa na mgeni rasmi kabla ya ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana Kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam.
PIX 17Vijana toka kundi la The Africa wakionesha igizo maalum linalohusu athari ya maradhi mbalimbali yakiwemo TB na Ukimwi yanayoweza kuwakumba vijana katika maisha yao ya ujana endapo hawatakuwa makini na jinsi gani ya kujiepusha nayo.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dar es Salaam
NDOA nyingi za utotoni husababishwa na tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kuwalazimisha watoto wao wa kike kuolewa katika umri mdogo kwa tamaa ya kujipatia fedha ama utajiri katika familia zao jambo ambalo linawanyima haki ya kusoma watoto wengi kwani watoto hawa wanakuwa wako katika umri chini ya miaka kumi na nane.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Wailesi Wilaya ya Temeke Bw. Abdul Kidege wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana linalofanyika kila mwisho wa mwezi katika kituo cha vijana UMATI jijini Dar es Salaam.
Bw. Kidege amesema kuwa kuna baadhi ya wazee na vijana wenye tabia ya kuwarubuni wasichana wadogo kwa kuwapa pesa na vitu vya thamani kwa lengo la kuwashawishi kuolewa nao na pia kuna baadhi ya wazazi ambao wakati mwingine ushirikiana katika kufanikisha azma hiyo jambo ambalo ni kinyume na haki za watoto katika jamii.
“Kuna baadhi ya wasichana wenye umri mdogo wamekuwa wakinyanyaswa kijinsia kwa kubakwa na wengine kulazimishwa na wazazi wao wenyewe kuolewa na watu wazima ambao wamewazidi umri, jambo hili halikubariki na vijana nawaasa msikubali kurubuniwa kwa pesa au vitu toka kwa watu wa namna hiyo”. Alisema Bw. Kidege.
Kwa upande wake Afisa Vijana Msaidizi Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI) Bi. Upendo Daud amewaeleza vijana waliohudhuria tamasha hilo kuwa vijana wanapohudhuria matamasha katika kituo cha UMATI wanapata fursa kubwa ya kupata elimu bure juu ya afya ya uzazi, athari za mimba za utotoni, kupima Ukimwi, ushauri nasaha, uzazi wa mpango pamoja na uelimishaji rika jambo ambalo linawafanya vijana wengi waweze kujitambua na kujikinga.
 “Hili ni Tamasha kwaajili ya vijana linaloandaliwa kila mwisho wa mwezi na Youth Action Movement (YAM) kwa lengo la kuwaelemisha vijana juu ya mambo mbalimbali yanayohusiana na afya na mada kuu ya tamasha hili kwa leo ni Ndoa za umri mdogo  na athari zake”. Alisema Bi. Upendo.
Youth Action Movement (YAM) ni kikundi cha Vijana ambacho kilianzishwa na chama cha uzazi na malezi bora Tanzania (UMATI) kwa ufadhili wa Internationa Planned Parenthood Federation (IPPF). Chama hiki cha vijana kinapatikana katika kila tawi la UMATI nchi nzima na kwa tawi la Dar es Salaam ndiyo waandaaji wa Jamvi la vijana kila mwezi ambapo husaidia kutoa huduma bure kwa vijana kuhusu afya ya uzazi, kupima Ukimwi, ushauri nasaha, uzazi wa mpango pamoja na uelimishaji rika

CHUO CHA MIPANGO DODOMA CHAIBUKA WASHINDI WA FAINAILI YA MPIRA WA KIKAPU ILIYOANDALIWA NA MH ANTONY MAVUNDE MJINI DODOMA,MWENYEKITI WA ASASI YA VIJANA YA "YES" AMPONGEZA ,

Fainali ya mashindano ya mpira wa kikapu yaliyoandaliwa na Mh Anton Mavunde yaliyofanyika weekend hii katika uwanja wa vijana mjini Dodoma na kufikia tamati siku ya jana 31/05/2014 ambapo vijana wa chuo cha Mipango waliibuka kidedea huku wakiondoka vifua juu baada ya kutwaa kombe la ushindi,

Mashindano hayo yalikuwa yakipekee sana yenye maandalizi ya hali ya juu sana ambapo Mgeni rasmi wa mashindano hayo alikuwa ni Mh Juma Nkamia pamoja na viongozi mbalimbali wa nchi na pia kulikuwa na werembo wa Miss Vyuo Vikuu vyote vya tanzania ambao walikuja kumuunga mkono kijana mwenzao Mh Antony Mavunde kwa kuandaa mashindano hayo,Huku warembo hao wakionyesha mbwembwe kidogo huku mashibiki wakifurahia kwa nderemo na vifijo kwa kupata burudani tofauti . Pia baadhi ya vijana walionekana kufurahishwa na mashindano hayo na kumpongeza sana Mh Anton Mavunde kwa kuwajali vijana na kuwakumbuka na kuwasaidia katika namna moja ama nyingine, HONGERA SANA MH ANTON MAVUNDE

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Youth Empowerment and Support (YES)  Bw. Remidius Emmanuel amempongeza  Bwana antony mavunde kwa kuwa mstari wa mbele   kujumuika katika shughuli mbalimbali za vijana hususani michezo.



































Saturday, May 31, 2014

FAINALI ZA MAVUNDE BASKETBALL TOURNAMENT 2014(MKOANI DODOMA)-NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA,UTAMA MAMICHEZO AWA MGENI RASMI

     Naibu Waziri Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Juma Nkamia akizungumza  na wachezaji kabla ya mchezo huo kuanza.

Fainali za Mavunde Basketball Tournament 2014  zimefanyika leo   na kuhudhuriwa na   Naibu Waziri Mh Juma Nkamia (Mgeni rasmi), Mbunge wa Sumbawanga Mjini Mh Aeshi, Mhe: Steven Masangia (Diwani wa kata ya Mnadani  na Mkurugenzi mtendaji wa  Kampuni ya Ebenezer Destefanos),Washiriki wa Miss Vyuo vikuu, Viongozi wa UVCCM Mkoa na Wilaya ya Dodoma. Fainali hizo zimefanyika  leo katika uwanja wa Vijana Youth Centre (Area C) Mjini Dodoma.
  

SOMA HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO, MHE. DKT. FENELLA E. MUKANGARA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2014/2015

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara yake kwa mwaka 2014/2015 mjini Dodoma jana. Waziri Mukangara ameomba Wizara yake iidhinishiwe kiasi cha Shilingi, 35,371,884,000 ambapo kati ya hizo jumla ya shilingi 20,371,884,000 ni za matumizi ya kawaida na kiasi kilichobaki ni fedha za miradi. 
---
HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO, MHE. DKT. FENELLA E. MUKANGARA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA  KWA MWAKA 2014/2015

A.    UTANGULIZI

1.   Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo kwenye Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii sasa naomba kutoa hoja ya kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Asasi zake kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.

2.   Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda na kunipa nguvu ya kutekeleza majukumu yangu na kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha bajeti hii.

3.   Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima nitumie fursa hii kuwapongeza Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa uongozi wao thabiti ambao umeendelea kudumisha amani na mshikamano wa Taifa letu. Tunajivunia pia matunda ya Waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao mwaka 2014 umetimiza miaka 50. Uongozi wao umetuwezesha kufikia maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa tuliyonayo hivi sasa.

HI NDIO HOTUBA YA MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI MHE: JOSEPH MBILINYI YA WIZARA YA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO 2014/2015

JOSEPH O. MBILINYI: HOTUBA YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015
(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013) 

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, napenda kuchuku nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema na kwa kunitumia kama chombo cha mabadiliko hasa katika kutetea haki za wanahabari, vijana, wanamichezo na wasanii. Namshukuru Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Mhe. Freeman A. Mbowe kwa kuendelea kuwa na imani nami katika kuisimamia Serikali katika wizara hii. Aidha, napongeza hatua ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuungana kwa pamoja kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania. Napongeza UKAWA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwaelimisha wananchi nchi nzima. Napenda kuchukua nafasi hii kutoa salamu za rambirambi kwa wasanii nchini kwa vifo vya waigizaji Adam Kuambiana na Rachel Haule vilivyotokea hivi karibuni. Mungu azilaze Roho za Marehemu mahali pema peponi. Amen!

Saturday, April 19, 2014

TUYAKEMEE MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA KWA VIJANA

Dar es Salaam. Utumiaji wa dawa za kulevya umekuwa tatizo kubwa linaloikumba dunia hasa wakati huu wa utandawazi, huku sehemu ya waathirika wakuu wa dawa hizo wakiwa vijana ambao ni nguvukazi ya taifa.
Vijana wengi wanaotumia dawa za kulevya wamekuwa wakieleza chanzo kikuu cha wao kujiingiza katika matumizi hayo ni kushawishiwa na marafiki zao na ugumu wa maisha.
Hapa nchini vita ya dawa za kulevya imekuwa kubwa kadri siku zinavyozidi kusonga mbele huku wahusika wakuu wakielezwa kuwa ni vijana. Kundi hili ambalo ni nguvukazi ya taifa, wamekuwa wakitumika kusafirisha sehemu mbalimbali za dunia na nyakati zingine wao wenyewe wakitumia.

Sunday, January 19, 2014

MAJIBU YA RAIS- KIKWETE AFANYA UTEUZI WA BAADHI YA MAWAZIRI NA MANAIBU




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-

OFISI YA RAIS
Hakuna mabadiliko.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi (Muungano) – Hakuna mabadiliko
Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)
Waziri wa Nchi (Mazingira).
Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)
Naibu Waziri

OFISI YA WAZIRI MKUU
Hakuna mabadiliko

WIZARA

WIZARA YA FEDHA
Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) – Waziri wa Fedha
Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb) – Naibu Waziri wa Fedha
Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)- Naibu Waziri wa Fedha

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)-Waziri wa Katiba na Sheria
Naibu Waziri – Hakuna mabadiliko

WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) – Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)- Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

WIZARA YA UJENZI
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)- Waziri wa Mambo ya Ndani
Naibu Waziri – Hakuna Mabadiliko

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)- Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)- Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Waziri: Hakuna mabadiliko
Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) – Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
Waziri: Hakuna mabadiliko
Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) – Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) – Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)- Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

WIZARA YA KAZI NA AJIRA
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
Waziri – Hakuna mabadiliko

Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb) – Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

WIZARA YA MAJI
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)- Naibu Waziri wa Maji

WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) – Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

WIZARA YA UCHUKUZI
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Waziri – Hakuna mabadiliko

Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) – Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)-Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)-Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Waziri – Hakuna mabadiliko
Naibu Waziri (Madini) – Hakuna mabadiliko

Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)

Naibu Waziri (Nishati)

Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI

Ikulu
DAR ES SALAAM

19 Januari, 2014

INAPENDEZA: MA-RAIS WA TAASISI ZA ELIMU YA JUU- DODOMA WAONYESHA USHIRIKIANO KWA VITENDO



 Baada ya Rais wa COBESO Mhe; Remidius M. Emmanuel kumchakaza mabao Rais wa UDOM Mhe; Hussein Mahamudu Rashidi ikawa moja ya urafiki wao wa kudumu, hii imetokea jana Jumamosi tarehe 18/01/2014 chuo cha UDOM kujakucheza na CBE na baadae chuo cha CBE kuibuka na ushindi. Rais wa UDOM ilimbidi aje kuwaona vijana wake akisindikizwa na Rais wa St.John Mhe; Edmond J. Katumbi na Rais wa chuo cha Madini Mhe; Lwitiko Steven , Ikiwa ndio muda mwafaka wa kuingia geti la chuo cha CBE Dodoma Campus Mhe; Remidius alifanya utambulisho wa viongozi hawa kwa wanafunzi na viongozi wa COBESO akianza na Mhe; Riziki Shaweji Waziri wa Fursa mipango na Uwezeshaji, na pia utambulisho uliendelea mpaka uwanjani. Naomba turejee kwa picha 
Mwanaripoti wetu Katibu Mkuu wa Habari na Mahusiano Mhe; Angelo Numvire
 Rais wa UDOM akipewa pole na wanafunzi wa chuo cha CBE kwa timu yake kupigwa magori hususani michezo yote.
 Rais wa St.John Mhe; Edmond J. Katumbi akiandika jina lake kwenye kitabu cha wageni office ya COBESO

Rais wa UDOM Mhe; Hussein Mahamudu Rashidi