Afisa
Msaidizi wa Vijana kituo cha UMATI tawi la Dar es Salaam Bi. Upendo
Daud akiwaeleza vijana kuhusu mada kuu ya Tamasha ambayo ni “Athari za
ndoa za utotoni” wakati wa ufunguzi wa tamasha la mwezi katika kituo
hicho.
Mwenyekiti
wa mtaa wa Wailes Bw. Abdul Kidege ambaye ndiye mgeni rasmi katika
Tamasha la Jamvi la vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam akitoa
hotuba yake fupi kwa vijana waliohudhuria tamasha hilo lenye lengo la
kuwaeleimisha vijana juu ya athari za ndoa za utotoni.
Vijana
wakifuatilia kwa makini hotuba ikiyotolewa na mgeni rasmi kabla ya
ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana Kituo cha UMATI jijini Dar es
Salaam.
Vijana
toka kundi la The Africa wakionesha igizo maalum linalohusu athari ya
maradhi mbalimbali yakiwemo TB na Ukimwi yanayoweza kuwakumba vijana
katika maisha yao ya ujana endapo hawatakuwa makini na jinsi gani ya
kujiepusha nayo.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dar es Salaam
NDOA
nyingi za utotoni husababishwa na tabia ya baadhi ya wazazi na walezi
kuwalazimisha watoto wao wa kike kuolewa katika umri mdogo kwa tamaa ya
kujipatia fedha ama utajiri katika familia zao jambo ambalo linawanyima
haki ya kusoma watoto wengi kwani watoto hawa wanakuwa wako katika umri
chini ya miaka kumi na nane.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Wailesi Wilaya ya Temeke Bw. Abdul
Kidege wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana linalofanyika
kila mwisho wa mwezi katika kituo cha vijana UMATI jijini Dar es Salaam.
Bw.
Kidege amesema kuwa kuna baadhi ya wazee na vijana wenye tabia ya
kuwarubuni wasichana wadogo kwa kuwapa pesa na vitu vya thamani kwa
lengo la kuwashawishi kuolewa nao na pia kuna baadhi ya wazazi ambao
wakati mwingine ushirikiana katika kufanikisha azma hiyo jambo ambalo ni
kinyume na haki za watoto katika jamii.
“Kuna
baadhi ya wasichana wenye umri mdogo wamekuwa wakinyanyaswa kijinsia
kwa kubakwa na wengine kulazimishwa na wazazi wao wenyewe kuolewa na
watu wazima ambao wamewazidi umri, jambo hili halikubariki na vijana
nawaasa msikubali kurubuniwa kwa pesa au vitu toka kwa watu wa namna
hiyo”. Alisema Bw. Kidege.
Kwa
upande wake Afisa Vijana Msaidizi Chama cha Uzazi na Malezi Bora
Tanzania (UMATI) Bi. Upendo Daud amewaeleza vijana waliohudhuria tamasha
hilo kuwa vijana wanapohudhuria matamasha katika kituo cha UMATI
wanapata fursa kubwa ya kupata elimu bure juu ya afya ya uzazi, athari
za mimba za utotoni, kupima Ukimwi, ushauri nasaha, uzazi wa mpango
pamoja na uelimishaji rika jambo ambalo linawafanya vijana wengi waweze
kujitambua na kujikinga.
“Hili
ni Tamasha kwaajili ya vijana linaloandaliwa kila mwisho wa mwezi na
Youth Action Movement (YAM) kwa lengo la kuwaelemisha vijana juu ya
mambo mbalimbali yanayohusiana na afya na mada kuu ya tamasha hili kwa
leo ni Ndoa za umri mdogo na athari zake”. Alisema Bi. Upendo.
Youth
Action Movement (YAM) ni kikundi cha Vijana ambacho kilianzishwa na
chama cha uzazi na malezi bora Tanzania (UMATI) kwa ufadhili wa
Internationa Planned Parenthood Federation (IPPF). Chama hiki cha vijana
kinapatikana katika kila tawi la UMATI nchi nzima na kwa tawi la Dar es
Salaam ndiyo waandaaji wa Jamvi la vijana kila mwezi ambapo husaidia
kutoa huduma bure kwa vijana kuhusu afya ya uzazi, kupima Ukimwi,
ushauri nasaha, uzazi wa mpango pamoja na uelimishaji rika

No comments :
Post a Comment