YOUTH EMPOWERMENT AND SUPPORT (YES) - NGO
Sunday, June 8, 2014
Thursday, June 5, 2014
PINDA ATEMBELEA SHULE YA WASIOONA YA BIGIRI CHAMWINO– DODOMA
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama baadhi ya michoro unayotumika katika
kuwafundishia wanafunzi wasiona wakati alipotombelea shule maalu ya
Wasioona ya Bigiri Dodoma Juni4,2014. Kulia ni Mratibu wa Mpango wa
kuifadhili shule hiyo, Bw. V. Ramadhar Reddy ambaye ni Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya SURA. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama baadhi ya michoro unayotumika katika
kuwafundishia wanafunzi wasiona wakati alipotombelea shule maalu ya
Wasioona ya Bigiri Dodoma Juni4,2014. Kulia ni Mratibu wa Mpango wa
kuifadhili shule hiyo, Bw. V. Ramadhar Reddy ambaye ni Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya SURA. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua majengo na vifaa vya kufundishia wakati
alipotembelea Shule Maalu ya Wasioona ya Bigiri iliyopo Dodoma Juni 4,
2014 Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Reheme Nchimbi Juni 4,
2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na walimu, baadhi ya wanafunzi na
watendaji wa wilaya ya Chamwino wakati alipotembelea shule ya
wasiiona ya Bigiri Juni 4, 2014, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Dr. Rehema Nchimbi na kulia ni Mratibu wa Mpango wa kuifadhili shule
hiyo, Bw. V. Ramadhar Reddy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Sunday, June 1, 2014
VIJANA WAASWA KUJIEPUSHA NA NDOA KATIKA UMRI MDOGO
Afisa
Msaidizi wa Vijana kituo cha UMATI tawi la Dar es Salaam Bi. Upendo
Daud akiwaeleza vijana kuhusu mada kuu ya Tamasha ambayo ni “Athari za
ndoa za utotoni” wakati wa ufunguzi wa tamasha la mwezi katika kituo
hicho.
Mwenyekiti
wa mtaa wa Wailes Bw. Abdul Kidege ambaye ndiye mgeni rasmi katika
Tamasha la Jamvi la vijana kituo cha UMATI jijini Dar es Salaam akitoa
hotuba yake fupi kwa vijana waliohudhuria tamasha hilo lenye lengo la
kuwaeleimisha vijana juu ya athari za ndoa za utotoni.
Vijana
wakifuatilia kwa makini hotuba ikiyotolewa na mgeni rasmi kabla ya
ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana Kituo cha UMATI jijini Dar es
Salaam.
Vijana
toka kundi la The Africa wakionesha igizo maalum linalohusu athari ya
maradhi mbalimbali yakiwemo TB na Ukimwi yanayoweza kuwakumba vijana
katika maisha yao ya ujana endapo hawatakuwa makini na jinsi gani ya
kujiepusha nayo.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO, Dar es Salaam
NDOA
nyingi za utotoni husababishwa na tabia ya baadhi ya wazazi na walezi
kuwalazimisha watoto wao wa kike kuolewa katika umri mdogo kwa tamaa ya
kujipatia fedha ama utajiri katika familia zao jambo ambalo linawanyima
haki ya kusoma watoto wengi kwani watoto hawa wanakuwa wako katika umri
chini ya miaka kumi na nane.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Wailesi Wilaya ya Temeke Bw. Abdul
Kidege wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Jamvi la Vijana linalofanyika
kila mwisho wa mwezi katika kituo cha vijana UMATI jijini Dar es Salaam.
Bw.
Kidege amesema kuwa kuna baadhi ya wazee na vijana wenye tabia ya
kuwarubuni wasichana wadogo kwa kuwapa pesa na vitu vya thamani kwa
lengo la kuwashawishi kuolewa nao na pia kuna baadhi ya wazazi ambao
wakati mwingine ushirikiana katika kufanikisha azma hiyo jambo ambalo ni
kinyume na haki za watoto katika jamii.
“Kuna
baadhi ya wasichana wenye umri mdogo wamekuwa wakinyanyaswa kijinsia
kwa kubakwa na wengine kulazimishwa na wazazi wao wenyewe kuolewa na
watu wazima ambao wamewazidi umri, jambo hili halikubariki na vijana
nawaasa msikubali kurubuniwa kwa pesa au vitu toka kwa watu wa namna
hiyo”. Alisema Bw. Kidege.
Kwa
upande wake Afisa Vijana Msaidizi Chama cha Uzazi na Malezi Bora
Tanzania (UMATI) Bi. Upendo Daud amewaeleza vijana waliohudhuria tamasha
hilo kuwa vijana wanapohudhuria matamasha katika kituo cha UMATI
wanapata fursa kubwa ya kupata elimu bure juu ya afya ya uzazi, athari
za mimba za utotoni, kupima Ukimwi, ushauri nasaha, uzazi wa mpango
pamoja na uelimishaji rika jambo ambalo linawafanya vijana wengi waweze
kujitambua na kujikinga.
“Hili
ni Tamasha kwaajili ya vijana linaloandaliwa kila mwisho wa mwezi na
Youth Action Movement (YAM) kwa lengo la kuwaelemisha vijana juu ya
mambo mbalimbali yanayohusiana na afya na mada kuu ya tamasha hili kwa
leo ni Ndoa za umri mdogo na athari zake”. Alisema Bi. Upendo.
Youth
Action Movement (YAM) ni kikundi cha Vijana ambacho kilianzishwa na
chama cha uzazi na malezi bora Tanzania (UMATI) kwa ufadhili wa
Internationa Planned Parenthood Federation (IPPF). Chama hiki cha vijana
kinapatikana katika kila tawi la UMATI nchi nzima na kwa tawi la Dar es
Salaam ndiyo waandaaji wa Jamvi la vijana kila mwezi ambapo husaidia
kutoa huduma bure kwa vijana kuhusu afya ya uzazi, kupima Ukimwi,
ushauri nasaha, uzazi wa mpango pamoja na uelimishaji rika
CHUO CHA MIPANGO DODOMA CHAIBUKA WASHINDI WA FAINAILI YA MPIRA WA KIKAPU ILIYOANDALIWA NA MH ANTONY MAVUNDE MJINI DODOMA,MWENYEKITI WA ASASI YA VIJANA YA "YES" AMPONGEZA ,
Mashindano hayo yalikuwa yakipekee sana yenye maandalizi ya hali ya juu sana ambapo Mgeni rasmi wa mashindano hayo alikuwa ni Mh Juma Nkamia pamoja na viongozi mbalimbali wa nchi na pia kulikuwa na werembo wa Miss Vyuo Vikuu vyote vya tanzania ambao walikuja kumuunga mkono kijana mwenzao Mh Antony Mavunde kwa kuandaa mashindano hayo,Huku warembo hao wakionyesha mbwembwe kidogo huku mashibiki wakifurahia kwa nderemo na vifijo kwa kupata burudani tofauti . Pia baadhi ya vijana walionekana kufurahishwa na mashindano hayo na kumpongeza sana Mh Anton Mavunde kwa kuwajali vijana na kuwakumbuka na kuwasaidia katika namna moja ama nyingine, HONGERA SANA MH ANTON MAVUNDE
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Youth Empowerment and Support (YES) Bw. Remidius Emmanuel amempongeza Bwana antony mavunde kwa kuwa mstari wa mbele kujumuika katika shughuli mbalimbali za vijana hususani michezo.
Saturday, May 31, 2014
FAINALI ZA MAVUNDE BASKETBALL TOURNAMENT 2014(MKOANI DODOMA)-NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA,UTAMA MAMICHEZO AWA MGENI RASMI
Naibu Waziri Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Juma
Nkamia akizungumza na wachezaji kabla ya mchezo huo kuanza.
Fainali za Mavunde Basketball Tournament 2014 zimefanyika leo na kuhudhuriwa na Naibu Waziri Mh Juma Nkamia (Mgeni rasmi), Mbunge wa Sumbawanga Mjini Mh Aeshi, Mhe: Steven Masangia (Diwani wa kata ya Mnadani na Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Ebenezer Destefanos),Washiriki wa Miss Vyuo vikuu, Viongozi wa UVCCM Mkoa na Wilaya ya Dodoma. Fainali hizo zimefanyika leo katika uwanja wa Vijana Youth Centre (Area C) Mjini Dodoma.
SOMA HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO, MHE. DKT. FENELLA E. MUKANGARA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2014/2015

Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Dk. Fenella Mukangara akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na
matumizi ya
fedha ya Wizara yake kwa mwaka 2014/2015 mjini Dodoma jana. Waziri
Mukangara ameomba Wizara yake iidhinishiwe kiasi cha Shilingi,
35,371,884,000 ambapo kati ya hizo jumla ya shilingi 20,371,884,000 ni
za matumizi ya kawaida na kiasi kilichobaki ni fedha za miradi.
---
HOTUBA YA WAZIRI WA
HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO, MHE. DKT. FENELLA E. MUKANGARA (MB), AKIWASILISHA
BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2014/2015
A. UTANGULIZI
1.
Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo kwenye
Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya
Jamii sasa naomba kutoa hoja ya kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na
kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo na Asasi zake kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.
2.
Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kutumia fursa hii
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda na kunipa nguvu ya kutekeleza majukumu
yangu na kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha bajeti
hii.
3.
Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima nitumie fursa hii
kuwapongeza Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, kwa uongozi wao thabiti ambao umeendelea kudumisha amani na
mshikamano wa Taifa letu. Tunajivunia pia matunda ya Waasisi wa Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar ambao mwaka 2014 umetimiza miaka 50. Uongozi wao
umetuwezesha kufikia maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa tuliyonayo hivi
sasa.
HI NDIO HOTUBA YA MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI MHE: JOSEPH MBILINYI YA WIZARA YA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO 2014/2015
JOSEPH O. MBILINYI: HOTUBA YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
HOTUBA
YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB)
KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA,
UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015
(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, napenda
kuchuku nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema na kwa
kunitumia kama chombo cha mabadiliko hasa katika kutetea haki za
wanahabari, vijana, wanamichezo na wasanii. Namshukuru Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Mhe. Freeman A. Mbowe kwa kuendelea kuwa na imani
nami katika kuisimamia Serikali katika wizara hii. Aidha, napongeza
hatua ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuungana kwa pamoja kwa maslahi
ya wananchi wa Tanzania. Napongeza UKAWA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya
kuwaelimisha wananchi nchi nzima. Napenda kuchukua nafasi hii kutoa
salamu za rambirambi kwa wasanii nchini kwa vifo vya waigizaji Adam
Kuambiana na Rachel Haule vilivyotokea hivi karibuni. Mungu azilaze Roho
za Marehemu mahali pema peponi. Amen!
Subscribe to:
Comments
(
Atom
)

Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua majengo na vifaa vya kufundishia wakati
alipotembelea Shule Maalu ya Wasioona ya Bigiri iliyopo Dodoma Juni 4,
2014 Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Reheme Nchimbi Juni 4,
2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
