kuza biashara yako

kuza biashara yako

Pages

Monday, August 19, 2013

SIMANZI: MWANAFUNZI MWINGINE WA CHUO CHA CBE AFARIKI DUNIA.

  MAREHEMU  SHIJA  MANYALILA


Ikiwa ni wiki chache tangu Chuo hiki cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Dodoma  kiondokewe na Mwanafunzi ( Marehemu Restuta Mayuma  mnamo Tarehe 05/08/2013) Chuo hiki kwa mara nyingine kimepata pigo kwa siku ya  jana (Tarehe 18/08/2013 siku ya Jumapili)  Mnamo saa 12 Asubuhi Baada ya Mwanafunzi wa Chuo Hicho  Ndugu  Shija  Manyalila Kufariki dunia baada ya kusumbuliwa  na Homa  pamoja na Malaria.
Akizungumza na Blogu yetu  Ndugu wa Marehemu Bw.Paschal  Amesema Marehemu  wiki chache zilizopita Alikuja Dodoma (Chuoni) kufanya Mitihani yake ya Supplimentary/Special  na kisha  kurudi makwao  Mkoani Shinyanga Eneo la Kolandoto  KM 40 kutoka Shinyanga Mjini kama unaelekea Mkoani Mwanza.Ambako hali yake ilibadilika mpaka kupelekea kifo chake.
Kwa mujibu  wa Bw. Paschal  amesema Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano  Tarehe  20/08/2013 Mkoani Shinyanga.

Mwanafunzi huyo aliyekuwa anasoma  Diploma ya Uhasibu  Mwaka wa kwanza  mkondo "C" kwa mwaka wa masomo 2012/2013, Ameibua simanzi miongoni Mwa wanafunzi wa Chuo hicho.

Blogu hii ilipojaribu kuzungumza na Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo cha CBE Kampasi ya Dodoma Amekiri kupata taarifa hizo na kwamba bado chuo kinaendelea kufanya taratibu zake kwa nafasi yake.

"TUNAWAOMBEA KWA  MUNGU NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WA  MAREHEMU  SHIJA  , MUNGU AWATIE NGUVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU"

AMINA.

No comments :

Post a Comment