kuza biashara yako

kuza biashara yako

Pages

Tuesday, August 6, 2013

MWANAFUNZI WA CBE KAMPASI YA DODOMA AFARIKI DUNIA (05/08/2013)


 
MAREHEMU    RESTUTA  MAYUMA

Ni masikitiko makubwa kwa wanafunzi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE)  kampasi ya Dodoma  kwa kumpoteza mwanafunzi mwenzao  Bi. Restuta Mayuma ambaye alifariki tarehe  05/08/2013 (Jumatatu) mnamo mishale ya saa kumi na moja jioni.
 Hata hivyo mwanafunzi huyo  alikuja dodoma kwa lengo la kufaya mitihani yake ( katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wa Chuo cha CBE  wamekuwa wakiendelea kufanya mitihani yao ya Special pamoja na ile ya Supplimentary.
Marehemu Restuta, Alikuwa anasoma Diploma , kozi ya Uhasibu (Accountancy) , ambapo alianza masomo ya Diploma mwaka wa masomo 2011/2012 na alitakiwa kuhitimu  Elimu yake  ya Diploma  mwaka 2012/213.Lakini  kwa kipindi hiki alikuja  chuo kurudia mitihani yake ya Diploma  I  .
Akizungumza  na Univesities Corner  Rafiki wa karibu sana na Mwanafunzi huyo (Marehemu Restuta)  alisema  Marehemu alikuwa anasumbuliwa na homa za hapa na pale (Malaria)  hali ambayo ilipelekea  mpaka kutokea kwa kifo chake.
 Tayari Mwili wake umesafirishwa leo kuelekea  Mkoani Dar es salaam eneo la BUNJU  kwa ajili ya shughuli za Mazishi ambapo  mwili huo umesafirishwa na Gari la Chuo (CBE)  Kwa kuambatana na  WARDEN, Mashauri Machunde (Mwanafunzi CBE)  pamoja na baadhi ya ndugu wa marehemu waliokuwepo mkoani Dodoma.

 Akizungumza kwa njia ya simu, Bw. Mashauri Machunde  (Mwanafunzi  CBE)  amewataka wanafunzi wote wa CBE wanaoishi jijini Dar es salaam kijitokeza katika mazishi ya  Mwanafunzi huyo   yanayotarajiwa kufanyika   kesho  nyumbani kwao "Bunju " Kwa kupanda magari yaendayo Bunju na kushukia eneo la Bunju "A" kituo  kinaitwa Shule au Hospital (Uliza kwa Mzee  Mayuma  karibu na Shule ya Sekondari Fanaka)
 Mwili wa Marehemu unatarajiiwa  kuagwa   mnamo saa 7 mchana (07/08/2013)  kabla ya shughuli za  Mazishi kuendelea.
  "Hii ni safari ya kila mmoja , Mwenzetu katangulia . Kwa masikitiko makubwa  Mmiliki wa Blog hii  Bw.Remidius Emmanuel  anatoa pole kwa Familia na ndugu jamaa na Marafiki waliofikwa na Msiba huo"

NOTE: 
Kwa wote walioko Dar es salaam  waweza kuwasiliana na Mashauri Machunde kwa namba : 0652-559011   ili kufika eneo  la msiba (BUNJU)


BAADHI YA PICHA ZA MAREHEMU  (RESTUTA  MAYUMA)  ENZI ZA UHAI WAKE

 


No comments :

Post a Comment