MAREHEMU SHIJA MANYALILA
Ikiwa ni wiki chache tangu Chuo hiki cha Elimu ya Biashara Kampasi ya Dodoma kiondokewe na Mwanafunzi ( Marehemu Restuta Mayuma mnamo Tarehe 05/08/2013) Chuo hiki kwa mara nyingine kimepata pigo kwa siku ya jana (Tarehe 18/08/2013 siku ya Jumapili) Mnamo saa 12 Asubuhi Baada ya Mwanafunzi wa Chuo Hicho Ndugu Shija Manyalila Kufariki dunia baada ya kusumbuliwa na Homa pamoja na Malaria.
Akizungumza na Blogu yetu Ndugu wa Marehemu Bw.Paschal Amesema Marehemu wiki chache zilizopita Alikuja Dodoma (Chuoni) kufanya Mitihani yake ya Supplimentary/Special na kisha kurudi makwao Mkoani Shinyanga Eneo la Kolandoto KM 40 kutoka Shinyanga Mjini kama unaelekea Mkoani Mwanza.Ambako hali yake ilibadilika mpaka kupelekea kifo chake.
Kwa mujibu wa Bw. Paschal amesema Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano Tarehe 20/08/2013 Mkoani Shinyanga.
Mwanafunzi huyo aliyekuwa anasoma Diploma ya Uhasibu Mwaka wa kwanza mkondo "C" kwa mwaka wa masomo 2012/2013, Ameibua simanzi miongoni Mwa wanafunzi wa Chuo hicho.
Blogu hii ilipojaribu kuzungumza na Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo cha CBE Kampasi ya Dodoma Amekiri kupata taarifa hizo na kwamba bado chuo kinaendelea kufanya taratibu zake kwa nafasi yake.
"TUNAWAOMBEA KWA MUNGU NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU SHIJA , MUNGU AWATIE NGUVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU"
AMINA.



