kuza biashara yako

kuza biashara yako

Pages

Sunday, May 5, 2013

MWANAFUNZI WA CBE DODOMA APATA AJALI, NI BAADA YA KUGONGWA NA GARI AINA YA NOAH).....

BW. ALFA SANGA    AKIENDELEA KUPATA MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA  AMANI (AREA  D)
 
Tarehe  03/05/2013  ( Ijumaa)  mnamo mishale ya saa 2  usiku, haitosaulika  Maishani mwa  Mwanafunzi  huyu  Alfa  Sanga  anaesoma   Cheti , course  ya Manunuzi na Ugavi  mkondo C (BCPS  "C") Katika chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi Ya Dodoma.
Akizungumza kwa kirefu,Bw. Emily  Mwandambo (Rafiki wa karibu wa Bw.alfa)  alisema ,   Ajali hiyo ilitokea  Maeneo ya Kibaoni  Area "E"   wakati Bw. Alfa  akiwa na wenzake  wakielekea chuoni  baada ya kufanya discussion na wenzake wanaoishi  Maeneo ya Flamingo.Hata hivyo  wakati  Bw. Alfa akivuka  barabara  (kibaoni -uwanja wa ndege)  Mara ilitokea  gari  aina ya Noah  ambayo ilimgonga  na kupelekea kuumia sana maeneo Kichwani  ambapo alichanika  kiasi flani kisha kuumia zaidi maeneo ya begani. Pamoja na hali hiyo dereva wa gari hilo hakusimama baada ya kubaini  kosa alilofanya.
 Hata hivyo  Mgonjwa huyo anaendelea kupata matibabu katika kituo cha Afya  AMANI  (AREA  " D")  Mpaka jana (04/05/2013  mishale ya saa 11 jioni ) Bw. Alfa alikuwa bado hajapata fahamu.
Universities Corner  inamuombea kwa Mungu  ili apate  kupona na kuendelea na masomo yake.    


     BW. REMIDIUS  EMMANUEL (KULIA)   AKIMJULIA HALI BW. ALFA   SANGA
  BAADHI YA  WANAFUNZI WA CBE   WAKIWA  KITUONI HAPO KWA AJILI YA KUMJULIA HALI MWANAFUNZI MWENZAO.

         MIONGONI MWA MARAFIKI WA KARIBU WA  BW. ALFA   SANGA
        UFAFANUZI UKITOLEWA  NA  NESI WA ZAMU, AKIFAFANUA  JAMBO JUU YA HALI YA MGONJWA.....

No comments :

Post a Comment