Chuo Cha Tumaini tawi la Dar es Salaam kimepata msiba wa mwanafunzi
wa mwaka wa kwanza aliekuwa anasoma sheria. Mwanafunzi Willhem Mushi
mkazi wa Moshi alipoteza maisha baada ya kujinyonga mpaka kufa
alipojifungia chumbani kwakeTarehe 29/04/2013 mida ya saa tano asubuhi. Mwili wa
marehemu uligundulika kuwa umekufa majira ya saa kumi alasiri chumbani
kwake. Mtoa taarifa ambae pia ni mwanafunzi mwenzake ametueleza kwa njia
ya simu.
Nini chanzo?!
Kuna taarifa za baadhi ya watu kuwa marehemu Willhem alifikia uamuzi
wa kujinyongaa mpaka kufa baada ya kutambua kuwa amefeli (disqualified)
masomo yake ya chuo. Sababu hii wengi bado wanaitilia mashaka.
Sababu nyingine ambayo imepata umaarufu zaidi ni ya kwamba marehemu
alikuwa akipata pesa kutoka bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu
yaani HESLB (wengi huliita BOOM) lakini hakuwaeleza wazazi wake kuwa
anapata pesa hizo. Kitendo hicho kilipelekea wazazi wa mwanafunzi huyu
kuwa anatumiwa pesa za matumizi na Ada kutoka kwa wazazi wake ili aweze
kuendesha maisha yake na kupata elimu ili iweze kumsaidi hapo mbeleni.
Marehemu anadaiwa kuwa alidanganya chuoni kwa mwalimu wake kuwa
amefiwa na dada yake kwahiyo hakuweza kufanya test za chuoni hapo
kitendo ambacho kilimlazimu mwalimu wake kumpa SPECIAL TEST.
Mzazi wa marehemu Willhem (Baba yake) aliamua kuja kumtembelea mwanae
hapo chuoni na kujua maendelea yake hapo ndipo mambo yalipooanza
kuharibika kwa ndugu yetu Willhem. Baba alipofika chuoni aligundua kuwa
mwanae bado anadaiwa ada na pia amekuwa akipata pesa za mkopo. Mzazi
yule pia alishangazwa na maendeleo mabaya ya mwanae hapo chuoni
kitaalumu lakini kubwa zaidi ni kupata taarifa ya kuwa WILLHEM HAKUFANYA
TEST KWAKUWA ALIFIWA NA DADA YAKE.
Dalili za kifo chake?
Inasemekana kuwa marehemu Willhem kwa kipindi cha zaidi ya mwezi
mmoja alikuwa akilalamika kuwa maisha ni magumu sana kwake na kuwa haoni
sababu za kuendelea kuishi. Haya maneno amekuwa akiyazungumza ambapo
wanafunzi wenzake wamekuwa wakishangazwa sana lakini hawakujua mwisho
wake itakuwa kwa Willhem kupoteza maisha kwa kujinyonga. Willhem alikuwa
akiishi maeneo ya Kurasini hapa jijini Dar es Salaam na wenzake watatu.
Polisi wanaendelea na uchunguzi kupata taarifa zaidi juu ya kifo cha
mwenzetu.
No comments :
Post a Comment