BW. ALFA SANGA AKIENDELEA KUPATA MATIBABU KATIKA KITUO CHA AFYA AMANI (AREA D)
Tarehe 03/05/2013 ( Ijumaa) mnamo mishale ya saa 2 usiku, haitosaulika Maishani mwa Mwanafunzi huyu Alfa Sanga anaesoma Cheti , course ya Manunuzi na Ugavi mkondo C (BCPS "C") Katika chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kampasi Ya Dodoma.
Akizungumza kwa kirefu,Bw. Emily Mwandambo (Rafiki wa karibu wa Bw.alfa) alisema , Ajali hiyo ilitokea Maeneo ya Kibaoni Area "E" wakati Bw. Alfa akiwa na wenzake wakielekea chuoni baada ya kufanya discussion na wenzake wanaoishi Maeneo ya Flamingo.Hata hivyo wakati Bw. Alfa akivuka barabara (kibaoni -uwanja wa ndege) Mara ilitokea gari aina ya Noah ambayo ilimgonga na kupelekea kuumia sana maeneo Kichwani ambapo alichanika kiasi flani kisha kuumia zaidi maeneo ya begani. Pamoja na hali hiyo dereva wa gari hilo hakusimama baada ya kubaini kosa alilofanya.
Hata hivyo Mgonjwa huyo anaendelea kupata matibabu katika kituo cha Afya AMANI (AREA " D") Mpaka jana (04/05/2013 mishale ya saa 11 jioni ) Bw. Alfa alikuwa bado hajapata fahamu.
Universities Corner inamuombea kwa Mungu ili apate kupona na kuendelea na masomo yake.

BW. REMIDIUS EMMANUEL (KULIA) AKIMJULIA HALI BW. ALFA SANGA
BAADHI YA WANAFUNZI WA CBE WAKIWA KITUONI HAPO KWA AJILI YA KUMJULIA HALI MWANAFUNZI MWENZAO.
MIONGONI MWA MARAFIKI WA KARIBU WA BW. ALFA SANGA
UFAFANUZI UKITOLEWA NA NESI WA ZAMU, AKIFAFANUA JAMBO JUU YA HALI YA MGONJWA.....



