kuza biashara yako

kuza biashara yako

Pages

Tuesday, November 19, 2013

YALIYOJILI KWENYE BONANZA LA MICHEZO ST.JOHN KWENYE MPIRA WA KIKAPU IKIAMBATANA NA VIDEO YAO....!


 Naibu waziri Bw. Masali Mnukwa akiwa na kocha Bw. Steven Shinji wakiwa wanaandaa kikosi chao cha mpira wa Kikapu. Hii ni bonanza la michezo ya kirafiki iliyofanyika St.John, katika mchezo huu wa kikapu Cbe ilicheza kwanguvu na kasi ikiwa vuta ni vute kwa kila pande zote. Baada ya mchezo huo Cbe ilipoteza  mechi hii.    
Hawa ni baadhi ya washabiki waliokuwepo kwenye mchezo wa kikapu st.John.
Wachezaji wakiwa wanakumbushana mbinu za mchezo huu.

HAWA NDIO WAHITIMU WA VYUO VYA ELIMU YA JUU WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI MWAKA 2013/2014 BAADA YA USAILI KUKAMILIKA



Maelekezo Muhimu.
1.Wahitimu wataondoka tarehe 19/11/2013 kwenda Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi, mabasi yataondoka Polisi Ufundi Dsm saa 06.00 asubuhi. Mwisho wa kuriporti Chuoni ni tarehe 23/11/2013. Atakayeripoti kuanzia tarehe 24.11.2013 atahesabika amechelewa hatapokelewa chuoni hapo.
 2.Vijana hawa watalazimika kufika chuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
a) Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
b) Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
c) Chandarua chenye upana futi tatu
d) Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
e) Pasi ya Mkaa
f) Ndoo moja
g) Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=). Aliyemwachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hatalazimika kulipia kiasi hiki cha fedha.
h) Pesa kidogo ya kujikimu.
3. Kwa mujibu wa kanuni za chuo ni marufuku kufika chuoni na simu ya mkononi au kifaa chochote cha mawasiliano. Atakayepatikana na simu atafukuzwa chuoni hapo. Chuo kitaelekeza na kusaidia kufanya mawasiliano.

4. Angalia orodha hapa chini;

WAHITIMU WA VYUO VYA ELIMU YA JUU WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI











Add caption