kuza biashara yako

kuza biashara yako

Pages

Wednesday, December 25, 2013

RAIS WA CBE AONGOZA WANAFUNZI WA CBE KATIKA KUTOA MKONO WA KHERI YA X MASS KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA- MIYUJI


 Mhe, Remidius M. Emmanuel (Rais wa Serikali ya wanafunzi CBE ya Dodoma) akiwa na baadhi ya viongozi katika kituo cha Watoto Yatimu cha Miyuji  tarehe 24/12/2013 mnamo saa tano asubuhi (jana), akitoa pongezi kwa Mlezi wa kituo hicho Sister Glory Shayo kwa kulea watoto hawa. Rais aliwasilisha baadhi ya vitu kwaajili ya watoto hao
 "Napenda tuwe mfano mzuri ndani na nje ya chuo, hata Mkoa kuwatembele watoto hawa kujiona nao ni sehemu ya jamii kiujumla" Maneno ya Rais.
VILIVYOTOLEWA NI;
Mchele kilo 50
Ngano kilo 50
Mafuta kula lita 20
Mafuta ya kujipata  dazan 1
Maji carton 2
Mhe, Yohana akimsikiliza Mhe, Remidius M. Emanuel  wakati wa kutoa  zawadi hizo
 Watoto hawa wakiongea na ndugu Dominicky Stephano na nyuso zao zikionekana ni za furaha 

 Waziri wa Fulsa na Mipango Mhe, Riziki Shaweji akiwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe, Simba

 Zawadi zilizo tolewa


 Mhe, Rais akikabidhi zawadi hizi kwa mlezi wa kituo hiki



 Rais akiwa na watoto hawa akionyesha upendo kwa watoto Yatima

 Hii ni nembo ya kituo hiki iyonacho sadifu mazingira harisi ya watoto wanolelewa mahari hapa.
 Mhe Ignas alipata bahati ya kutembelea shamba la mboga mboga hili ni shamba ambalo kituo kimeweza kuliwekeza kwa ajili ya kilimo hiki cha mboga mboga:

 Hakuna mahari popote duniani panapoweza kuondokana na janga la njaa pasipo kuwekeza katika kilimo vivyo hivyo hivyo katika kituo hiki wameamua kupigana na adui njaa kwa kujiandalia mazao yao: Tazama mashamba haya:

Saturday, December 14, 2013

HUYU NDIYE MWENYEKITI MPYA WA TAHLISO 2013/2014



   Bw, Musa  Mdede -Rais waChuo kikuu cha Bugando   (Katikati) Akizungumza Mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti  wa TAHLISO 2013/2014

Bw.Musa Mdede ameibuka Kidedea katika hatua ya pili baada ya kupata kura 18, akifuatiwa  na Rais wa  St. John  Dodoma Bw, Katumbi Edmund  kupata kura 7 akifuatiwa  na Bw.Hemed Ally Rais wa IFM aliyepata kura 6.
Ingwa katika hatua ya kwanza wagombea wa nafasi hiyo walikuwa  ni Watano,Ambapo matokeo yao ya awali   Musa Mdede  (Kura 16),Hemed Ally (kura 7) ,Katumbi Edmund (Kura  5) ,Bi. Tusubilege  Benjamin (Makamu wa Rais wa UDSM -Kura 3) na paschal  Mlela(  kutoka chuo cha Theophilo Kisanje  Mbeya -  kura  3) .Hali hiyo ilifanya  jumla ya kura kuwa 34   na kati ya wagombea wote katika hatua ya kwanza hakuna aliyefikisha  zaidi ya asilimi Hamsini (50%)  hivyo kuufanya uchaguzi kurudiwa katika nafasi hiyo kwa washindi watatu wakwanza katika hatua ya pili.

 Muonekano wa Viongozi wapya wa TAHLISO 2013/2014,kutoka kulia ni Mhazini  Bw.Mollel Hilary (Kutoka Chuo cha Kodi Dae es salaam),Bi.Halima Bakari -Katibu Mkuu(Kutoka chuo cha AMUCTA-Tabora),Makamu Mwenyekiti  Bw.Abdul Mohamed (Rais wa Chuo cha kikuu Zanzibar),Mwenyekiti  Bw.Musa  Mdede (Rais Chuo kikuu Bugando) na Naibu Mhazini  Bw.Khamis  Hamza (kutoka Chuo kikuu cha Zanzibar)


 
 Mwenyekiti  Anayemaliza Muda wake Bw. Amon  Chakushemeire   akizungumza  maneno machache baada ya  Mwenyekiti mpya kutangazwa.

HAWA NI BAADHI YA WANAO WANIA NAFASI YA MWENYEKITI WA TAHLISO 2013/2014

  Bw.  Katumbi  Edmund .J   Rais wa St. John Dodoma

 Bi. Tusubilege  Benjamin  Makamu wa Rais  Chuo kikuu cha Dar es saalam
 Bw. Hermed   Ally  (Kushoto) Rais wa IFM
                                Bw.Musa Mdede  (Kulia) Rais wa Chuo cha  Bugando

HII NDIO TUME YA KURATIBU UCHAGUZI WA TAHLISO 2013/2014


        Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi  ya TAHLISO  wakiwa katika picha ya Pamoja
  Mwenyekiti wa Muda aliyeratibu upatikanaji wa tume  Bi. Teddy  Ladislaus   ( Makamu wa Rais wa  Chuo cha Mzumbe) akihitimisha  zoezi hilo hapo jana.
    Mwenyekiti wa Muda aliyeratibu upatikanaji wa tume  Bi. Teddy  Ladislaus   ( Makamu wa Rais wa  Chuo cha Mzumbe) akisalimiana na Katibu wa Tume ya uchaguzi Bi. Fatma Othman , Katikati ni  Mwenyekiti wa Tume hiyo Bw.Mansou Mshauri.
 
    Mwenyekiti wa Tume Bw.Mansou Mshauri. akizungumza  na  wajumbe wa Mkutano mkuu  wa TAHLISO
   Tume iliyochaguliwa ikiwa  mbele ya Mwenyekiti wakati wa kula kiapo kabla ya kuanza kazi hapo jana

Thursday, December 12, 2013

VIKAO VYA TAHLISO VIMEANZA RASMI JANA (11/12/2013)KATIKA CHUO KIKUU CHA BUGANDO MWANZA

 Rais wa Chuo cha Elimu ya Biashara  (CBE) Kampasi ya Dodoma  Bw. Remidius  Emmanuel (wa kwanza kutoka kulia) akifuatilia mwenendo wa kikao hicho,Pembeni ni Bw. Antony Mapande Rais wa chuo kikuu cha Hubert   Kairuki Memorial.
 Katibu mkuu wa TAHLISO Donati Salla akiwasilisha taarifa ya utendaji  ya mwaka mzima katika kikao hicho cha 'Senate' kilicho jumuisha  Marais wa vyuo vikuu na Taasisi za Elimu ya juu nchini Tanzania.
 Rais wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwl  Nyerere  Bi. Eshe  Mzee  (aliyesimama)  akichangia  taarifa iliyosomwa na Katibu mkuu wa TAHLISO

 Muonekano wa meza  kuu,iliyojumuisha  viongozi wa TAHLISO
  Mwenyekiti wa TAHLISO  Bw. Amon  Chakushemeire   akizungumza na wajumbe wa mkutano wa  SENATE
    Makamu wa Rais Chuo kikuu cha  UDOM  Bw. Mahamudu  Rashidi  Hussein  (wa kwanza  kutoka kulia) akifuatilia kwa umakini  mwenendo wa kikao  hicho.                       
                                                      Baadhi ya  Ma-Rais wa vyuo mbalimbali

Monday, December 9, 2013

PROFESSOR EMANUEL MJEMA AZUNGUMZA NA WANAFUNZI WA CBE KAMPASI YA DODOMA.


 Tarehe 6/12/2013 siku ya  ijumaa Mkuu waChuo cha Elimu ya Biashara  (CBE) Professor Emmanuel  Mjema  anaanza kwa kukutana na Serikali ya wanafunzi ya CBE kampasi ya Dodoma (COBESO)  Ikiongozwa na Mhe: Remidius Emmanuel  .
Akizungumza na Serikali ya Wanafunzi  Mkuu wa Chuo huyo alianza kwa  kupongeza serikali ya wanafunzi na kisha  kutoa majibu ya hoja za msingi zilizotolewa na  Viongozi wa Serikali za wanafunzi.Kwa upande wake  Rais wa Serikali ya wanafunzi alitumia utaratibu wa kuwakaribisha baadhi ya viongozi COBESO   ambapo kila mmoja aliweza kutoa  kile ambacho alidhani ni sehemu ya shauku kwa wanafunzi wa cbe.Baadhi ya mambo ya msingi yaliyozungumzwa ilikuwa ni pamoja na  Utaratibu wa Assesment Plan,Suala la uwepo wa Huduma ya kwanza Chuoni,Uboreshwaji wa Transcript,ufinyu wa  vyumba vya kusomea,umuhimu wa Maktaba  ambayo itakidhi mahitaji ya wanafunzi,Tatizo la Utunzaji wa kumbukumbu,Prospectus na mambo mengine mengi ya namna hiyo.
Akijibu  hoja hizo mkuu huyo alisema suala la  Maktaba  ni muhimu ingawa  alijaribu kuishauri Serikali ya COBESO  Kuwashauri wanafunzi kufikiri zaidi kusoma vitabu kupitia njia ya mtandao,Hata hivyo Mkuu huyo wa Chuo alionyesha kuleta matumaini kwa  chuo hicho baada ya kusema sasa shughuli za matokeo ya mtihani sasa  zitafanyika kupitia Mfumo wa SARIS hatua ambayo itasaidia pia katika utunzaji wa kumbukumbu kikamilifu.Akizungumza juu ya Uwepo wa huduma ya kwanza amesema suala hilo liko wazi na wala halipingiki  na aliahidi kulifanyia kazi mara moja kupitia Mkurugenzi wa Kampasi ya Dodoma  Mhe; Mahimbo.
Suala la Transcript  alisema 'Alikubaliana  kwamba zipo sababu za msingi za kuhakikisha baadhi ya mabadiliko yanafanyiwa kazi  ili kuleta ubora wa transcript hizo'
Baada ya kuzungumza na Serikali ya wanafunzi alikwenda katika ukumbi wa chuo 'New Hall' ambapo alizungumza na wanafunzi wote.Moja kati ya mambo yaliyomshangaza mkuu huyo wa chuo ni pale  alipoona kila swali lililokuwa linaulizwa na wanafunzi lilikuwa ni miongoni mwa maswali   muhimu ambayo yalikuwa yamezungumzwa katika  kikao cha Prof Mjena na COBESO.
Licha ya kuzungumzia suala la Kupanda kwa ADA  Bado wanafunzi walionyesha kuhitaji kupata  maelezo zaidi,Mambo mengine yaliyozungumzwa na Mkuu huyo wa chuo ilikuwa ni pamoja na  kuwafahamisha wanafunzi kwamba tayari chuo cha CBE kimewisha jenga mahusiano na vyuo vingine  kama  Eastern Finlan University .

   Rais wa COBESO  Mhe; Remidius Emmanuel  akizungumza  kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Chuo
   Mkurugenzi wa Kampasi ya Dodoma  Mhe: G.Mahimbo  akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo

                      Wanafunzi wakiendelea kumsikiliza Mkuu wa Chuo Professor Mjema
                    Professor akiendelea na Mazungumzo......





                Maswali kutoka kwa Wanafunzi