kuza biashara yako

kuza biashara yako

Pages

Saturday, May 31, 2014

FAINALI ZA MAVUNDE BASKETBALL TOURNAMENT 2014(MKOANI DODOMA)-NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA,UTAMA MAMICHEZO AWA MGENI RASMI

     Naibu Waziri Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Juma Nkamia akizungumza  na wachezaji kabla ya mchezo huo kuanza.

Fainali za Mavunde Basketball Tournament 2014  zimefanyika leo   na kuhudhuriwa na   Naibu Waziri Mh Juma Nkamia (Mgeni rasmi), Mbunge wa Sumbawanga Mjini Mh Aeshi, Mhe: Steven Masangia (Diwani wa kata ya Mnadani  na Mkurugenzi mtendaji wa  Kampuni ya Ebenezer Destefanos),Washiriki wa Miss Vyuo vikuu, Viongozi wa UVCCM Mkoa na Wilaya ya Dodoma. Fainali hizo zimefanyika  leo katika uwanja wa Vijana Youth Centre (Area C) Mjini Dodoma.
  

SOMA HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO, MHE. DKT. FENELLA E. MUKANGARA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2014/2015

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara yake kwa mwaka 2014/2015 mjini Dodoma jana. Waziri Mukangara ameomba Wizara yake iidhinishiwe kiasi cha Shilingi, 35,371,884,000 ambapo kati ya hizo jumla ya shilingi 20,371,884,000 ni za matumizi ya kawaida na kiasi kilichobaki ni fedha za miradi. 
---
HOTUBA YA WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO, MHE. DKT. FENELLA E. MUKANGARA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA  KWA MWAKA 2014/2015

A.    UTANGULIZI

1.   Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo kwenye Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii sasa naomba kutoa hoja ya kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Asasi zake kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.

2.   Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda na kunipa nguvu ya kutekeleza majukumu yangu na kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha bajeti hii.

3.   Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima nitumie fursa hii kuwapongeza Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa uongozi wao thabiti ambao umeendelea kudumisha amani na mshikamano wa Taifa letu. Tunajivunia pia matunda ya Waasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao mwaka 2014 umetimiza miaka 50. Uongozi wao umetuwezesha kufikia maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa tuliyonayo hivi sasa.

HI NDIO HOTUBA YA MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI MHE: JOSEPH MBILINYI YA WIZARA YA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO 2014/2015

JOSEPH O. MBILINYI: HOTUBA YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2014/2015
(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013) 

UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, napenda kuchuku nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya njema na kwa kunitumia kama chombo cha mabadiliko hasa katika kutetea haki za wanahabari, vijana, wanamichezo na wasanii. Namshukuru Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Mhe. Freeman A. Mbowe kwa kuendelea kuwa na imani nami katika kuisimamia Serikali katika wizara hii. Aidha, napongeza hatua ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuungana kwa pamoja kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania. Napongeza UKAWA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwaelimisha wananchi nchi nzima. Napenda kuchukua nafasi hii kutoa salamu za rambirambi kwa wasanii nchini kwa vifo vya waigizaji Adam Kuambiana na Rachel Haule vilivyotokea hivi karibuni. Mungu azilaze Roho za Marehemu mahali pema peponi. Amen!