kuza biashara yako

kuza biashara yako

Pages

Sunday, January 19, 2014

MAJIBU YA RAIS- KIKWETE AFANYA UTEUZI WA BAADHI YA MAWAZIRI NA MANAIBU




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-

OFISI YA RAIS
Hakuna mabadiliko.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi (Muungano) – Hakuna mabadiliko
Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)
Waziri wa Nchi (Mazingira).
Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)
Naibu Waziri

OFISI YA WAZIRI MKUU
Hakuna mabadiliko

WIZARA

WIZARA YA FEDHA
Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb) – Waziri wa Fedha
Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb) – Naibu Waziri wa Fedha
Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)- Naibu Waziri wa Fedha

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)-Waziri wa Katiba na Sheria
Naibu Waziri – Hakuna mabadiliko

WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb) – Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)- Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

WIZARA YA UJENZI
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)- Waziri wa Mambo ya Ndani
Naibu Waziri – Hakuna Mabadiliko

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)- Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)- Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Waziri: Hakuna mabadiliko
Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb) – Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
Waziri: Hakuna mabadiliko
Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb) – Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb) – Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)- Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

WIZARA YA KAZI NA AJIRA
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
Waziri – Hakuna mabadiliko

Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb) – Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

WIZARA YA MAJI
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)- Naibu Waziri wa Maji

WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
Waziri – Hakuna mabadiliko
Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb) – Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

WIZARA YA UCHUKUZI
Hakuna mabadiliko

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Waziri – Hakuna mabadiliko

Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb) – Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)-Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)-Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Waziri – Hakuna mabadiliko
Naibu Waziri (Madini) – Hakuna mabadiliko

Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)

Naibu Waziri (Nishati)

Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI

Ikulu
DAR ES SALAAM

19 Januari, 2014

INAPENDEZA: MA-RAIS WA TAASISI ZA ELIMU YA JUU- DODOMA WAONYESHA USHIRIKIANO KWA VITENDO



 Baada ya Rais wa COBESO Mhe; Remidius M. Emmanuel kumchakaza mabao Rais wa UDOM Mhe; Hussein Mahamudu Rashidi ikawa moja ya urafiki wao wa kudumu, hii imetokea jana Jumamosi tarehe 18/01/2014 chuo cha UDOM kujakucheza na CBE na baadae chuo cha CBE kuibuka na ushindi. Rais wa UDOM ilimbidi aje kuwaona vijana wake akisindikizwa na Rais wa St.John Mhe; Edmond J. Katumbi na Rais wa chuo cha Madini Mhe; Lwitiko Steven , Ikiwa ndio muda mwafaka wa kuingia geti la chuo cha CBE Dodoma Campus Mhe; Remidius alifanya utambulisho wa viongozi hawa kwa wanafunzi na viongozi wa COBESO akianza na Mhe; Riziki Shaweji Waziri wa Fursa mipango na Uwezeshaji, na pia utambulisho uliendelea mpaka uwanjani. Naomba turejee kwa picha 
Mwanaripoti wetu Katibu Mkuu wa Habari na Mahusiano Mhe; Angelo Numvire
 Rais wa UDOM akipewa pole na wanafunzi wa chuo cha CBE kwa timu yake kupigwa magori hususani michezo yote.
 Rais wa St.John Mhe; Edmond J. Katumbi akiandika jina lake kwenye kitabu cha wageni office ya COBESO

Rais wa UDOM Mhe; Hussein Mahamudu Rashidi