BW. MIRAJI SIMBA - MAKAMU WA RAIS KWA MGOMBEA MAXIMILIAN ( CBE DODOMA 2013/2014)
Akizungumza na chanzo chetu cha habari Moja kati ya Wagombea wa kinyang'anyiro cha Urais CBE-Dodoma Bw. Miraji Simba ambaye ni mgombea Mwenza (makamu wa Rais) wa Maimiliani ,Ameibuka na kuitaka jamii ya wana CBE kuondoa tofauti mbalimbali na kudumu kama ndugu jamaa na Marafiki hasa katika nyanja za kitaaluma.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu vuguvugu la uchaguzi kupungua kasi hasa baada ya Moja ya Wagombea wa nafasi ya Urais Bw. Dotto Kazi Leonard kuishitaki Maha
kamani tume pamoja na Bodi ya Chuo kwa kwa madai ya kutotendewa haki juu ya kuondolewa kwake katika kinyang'anyiro hicho.
Katika hatua nyingine Bado Bw. Remidius Emmanuel Ameendelea kung'ara na kukubalika kama mkombozi mkuu wa jamii ya wana CBE kufuatia uwezo na historia aliyonayo katika nyadhifa alizo wahi kuongoza katika vyuo mbalimbali hapa Tanzania.
Maamuzi ya Mahakama yamekuwa yakisubiliwa kwa hamu kubwa ingawa kumekuwepo na hali ya wasiwasi kwa wanafunzi walio wengi kwa kuamini kuwa huenda uchaguzi usifanyike tena. Akizungumza kwa Masharti ya kutotaja jina Mwanafunzi mmoja amesema wao kama wanafunzi wanayo haki ya kuwa na uongozi kupitia njia ya kidemokrasia na hivyo wanaamini Professor Mjema atalisimamia suala hilo.
