MR.Leonard L. Sylvester
MR.Leonard L. Sylvester, Ni mwanachuo wa chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma ambaye amethubutu kutunga kitabu chenye jina la " WAWEZA KUWA VILE UTAKAVYO" hatua inayomfanya kuanza kutimiza ndoto zake katika hatua za awali.Bw. Leonard anaonekana kijana mwenye kujiamini na kwamba hapa duniani kila kitu kinawezekana kama ukitia nia ya dhati kwa kuwa na malengo ya kile utarajiacho kufanya. Universities Corner ilikutana na Mwanachuo huyu na kutaka kujua jinsi alivyo weza kuanza au kupata wazo hili. Leonard anasema:-
WAWEZA KUWA VILE
UTAKAVYO Ni kitabu nilichoandika kinachohusu kujitambua kwa mtu
kuwa anaweza kuwa vile atakavyo katika maisha yake pasipo kuangalia amezaliwa
katika mazingira yapi au anapitia mazingira yapi.
Ndani ya kitabu hiki utapata kufahamu mambo mengi ambayo
yanagusa maisha ya mtu binafsi, katika maisha yake, changamoto anazokabiriana
nazo na njia au mbinu za kuzikabiri changamoto na kufikia pale alipo azimia
kufika kwa msaada wa Mungu.
·
Ndani ya kitabu hiki
utapata kufahamu kuwa ndani yako unao uwezo wa kuumba au kufanya jambo lolote hapa
duniani.
·
Utapata kufahamu
vizuizi unavyopata katika kuyaendea mafanikio yako.
·
Umuhimu wa kuyaombea
mafanikio yako.
Muonekano wa cover la kitabu hicho
HISTORIA FUPI YA KATIKA
KUKIANDIKA HIKI KITABU
Kwanza natanguliza shukrani zangu kwa Mungu kuniwezesha
na kunifanikisha mpaka kukiandika hiki kitabu na kikawa msaada mkubwa kwa
jamii.
Siku ya kwanza nilipopata wazo la kuandika kitabu
nilikuwa nimemaliza form four mwaka 2006 kipindi hicho nilikuwa nina shahuku
nifanye jambo gani ambalo litakuwa msaada kwa jamii inayonizunguka. Siku moja
nilikuwa kwenye semina ya Neno la Mungu Kanisani ninaposali, Mtumishi mmoja wa
kimataifa aitwaye DR. TAYO kutoka
Uingereza alikuwa akifundisha kuhusu kufanya jambo la kipekee ambalo jamii
itafaidika na hata ukifa utakumbukwa kwa hilo jambo ulilofanya.
Hapo ndio nikapata wazo la kuandika kitabu. Binafsi
napenda kufanikiwa na kuwa mtu wa tofauti kila mahali niendapo. Ndipo nikapata
wazo la kuandika kuhusu mafanikio. Nilianza kuandika hiki kitabu mwaka 2009,
nilitumia miaka mitatu kukiandika hiki kitabu hadi mwaka huu 2012 ndo
nilikikamilisha.
Haikuwa rahisi kuandika kitabu kama unavyofikiria, ni
kwa neema ya Mungu tu. Maana changamoto ni nyingi,
BAADHI YA CHANGAMOTO
NILIZOPOTIA.
1. Niliandika mpaka karatasi 17 Laptop iliharibika na data
zote zikapotea ikabidi nianze upya, sikukata tamaa, maana nilidhamiria toka
moyoni kuandika kitabu.
2. Kukatishwa tamaa na watu kuwa hauwezi kuandika kitabu
kwa sababu mimi ni kijana mdogo.
3. Pia na wengine walisema kitabu hakitawafikia wengi kwa sababu
sijulikani kwa watu.
Lakini mimi sikuangalia waliyosema bali niliangalia
moyoni mwangu nimedhamiria kuandika kitabu ili jamii ipate kujua maarifa
niliyonayo katika Yesu Kristo kwa habari ya mafanikio ya mtu na kujitambua kwa
mtu kuwa anaweza kuwa vile atakavyo katika maisha yake.
Maana nilijitambua kuwa NAWEZA KUWA VILE NITAKAVYO
na siyo mtu mwingine atakavyo.
Namshukuru Mungu alinipigania mpaka nikafika hatua ya
kuki-publish na mpaka sasa kitabu kinapatikana Bookshops, na watu washavipata.
Pia namshukuru Mungu napigiwa simu na watu wakimtukuza
Mungu kwa kuguswa katika maishha yao kupitia kukisoma hiki kitabu pia
nimeshaitwa kuendesha semina Dar es Salaam kuhusu hiki kitabu kwenda kufundisha
vijana.
Watu wengi wamebadilishwa maisha yao, fikra zao, mitazamo
yao baada ya kukisoma hiki kitabu.
Kwa hiyo ni jambo la kumtukuza Mungu kufikia hatua hii maana
nilijitambua kuwa naweza kufanya jambo lolote nikiamua.
USHAURI WANGU KWA
VIJANA WOTE, WANACHUO.
Jambo la muhimu sana la kufanya kwanza ni KUJITAMBUA. Jitambue kuwa wewe ni mtu
wa tofauti sana na ni wakipekee kuliko mtu mwingine yeyote maana kama Mungu
angetuumba wote sawa, basi kulikuwa hakuna haja ya wewe kuwepo duniani.
Mungu amekuleta hapa duniani akakufanya wa tofauti, ili
uweze kufanya mambo ya tofauti katika jamii ili jamii ikawe ya tofauti.
(Ngoja nikupe mfano wa kibiologia ili uone
kuwa wewe wa pekee)
Utaona aibu ila ndiyo ukweli wenyewe; weka maanani.
Mwanaume anazalisha mbegu za kiume milioni kwa siku na siku mimba yako inatungwa zilikuwa mbegu
nyingi zilitoka lakini mbegu ya kiume moja tu ikawahi kuingia kwenye yai la
mwanamke, ndo wewe ukazaliwa, na kumbuka mbegu nyingine pia wale walikuwa watu
lakini Mungu akaona wewe ndo uje duniani, je hile mbegu ya kiume ambayo ni wewe
isingewahi kwenye yai je ungukuwepo leo? (Hebu jiulize hilo swali).
Hapo ndiyo utakapojua kuna umuhimu wa wewe kuwepo hapa
duniani kwa ajili ya kusudi maalum.pia hupo hapa chuo kwa kusudi maalum hausomi
kwa sababu wazazi wamekuleta kusoma bali lipo kusudi la wewe kuwa hapa chuo
kusoma.
Vijana wenzangu, haijalishi unaishi mazingira ya namna
gani tambua kuwa unaweza kufanya jambo lolote katika maisha yako kama ukiamua.
Usijidharau kama una wazo la kuandika kitabu anza taratibu, kitabu hakiandikwi
siku moja, anza taratibu, kama wewe unataka kufanya biashara wakati unasoma
anza hakuna anayekuzuia (You can do int)
amun kufanya jambo
(STOP DREAMING JUST MAKE IT HAPPEN)
Kuwa na matarajio ambayo unajua utaweza kuyatimiza.
SIRI YA KUFANIKIWA
KATIKA UJANA WAKO
1. Penda kujitamkia mawazo mema(Think positive) hata kama mazingira magumu na jitamkie kuwa unaweza
kuwa vile utakavyo. Katika masomo yako jitamkie kuwa wewe ni mshindi na siyo
kushindwa hata kama hauelewi darasani. Siku zote kumbuka kinywa kinaumba na
Neno la Mungu linasema AWAZAVYO MTU NAFSINI MWAKE NDIVYO ALIVYO.
Kwa hiyo ulivyo sahivi ni matokeo ya ulikuwa
unajiwaziaje kipindi cha nyuma.
2.
Penda kusoma vitabu vya watu waliofanikiwa.
Jenga tabia ya kusoma vitabu. Kuna msemo wanasema (If you want to hide a black people something
write it in the book).
Jiulize mpaka sasa umesoma vitabu vingapi ukiachana na
vya darasani. Uwe na tabia ya kusoma vitabu ujue mbinu za kufanikiwa na kuwa wa
tofauti ili kila mtu akuonapo amtukuze Mungu na awe na shauku ya kuwa watofauti
na yeye.
Mimi ninapenda sana kusoma vitabu na ukitaka uhakika
uliza marafiki zangu wa karibu watakuambia. Nyumba nakaribia kufungua home
library kwenye room yangu kwa vitabu nilivyonavyo vya Kiswahili na kiingereza,
napenda kusikiliza mahubiri kwa watu waliofanya mambo makubwa hapa duniani.
Kwa kufanya hivyo nimepata kujitambua na kuwa wa tofauti
na yapo mambo makubwa nitaenda kuyafanya mbeleni.
3.
Penda kuwa na marafiki wenye akili
Kuna msemo unasema (Show me your friend and I will fell your
who you are). Je marafiki zako ulionao wanakufanya usonge mbele? Au
wanakurudisha nyuma? Ebu kuwa na marafiki ambao mkikaa dakika 5 unakuwa ume-gain
jambo la kimaisha na siyo kukaa na kupiga porojo.
Mimi watu ninaoshirikiana nao mambo ya ndani sana katika
maisha ni watu walionipita umri pia wanajitambua wao ni akina nani. Kwahiyo Napata
maarifa kiasi kwamba nikifanyia kazi maarifa niliyopata popote nitakapokwenda
ninakuwa wa tofauti.
4.
Penda kuandika malengo yako kwenye Notebook.
Vijana wengi wanapenda kuwish (I wish to have a good house, I wish to have
a good wife, I wish to have a nice job). Siyo vibaya ku-wish swali linakuja how
will you do to reach of what your wishing for? Hilo ndo tatizo la vijana wengi.
(Stop wish, just make it happen).
Ukiwa na tabia ya kuandika yale unayo-wish ni rahisi
kuyafuatilia ni namna gani ufanye ili kuyafikia malengo yako, na pia itakupa
wahisi kutaombea malengo yako.
NOTE:
Vijana wenzagu tuache mambo ya kuigaiga hebu amua kuwa
mtu halisi, jikubali (Proud yourself) maisha ya kuiga hayapendezi bali kuwa
vile Mungu anataka uwe, watu wakikucheka usione aibu ni bora wakakucheka lakini
umejitambua ulivyo kuliko kuiga ukaonekana kituko.
Tatizo la Waafrika na Watanzania (WE ARE SUMMARIZE A SUMMARIZED
SUMMARY)
Amua kuwa wa tofauti na utaweza kuwa vile utakavyo.
Mungu wangu awabariki sana.
Ukihitaji kitabu wasiliana na mimi.
Leonard L. Sylvester (Facilitator)
BBA I
0768
089000
leonardsylvester@yahoo.com